November 24, 2024

Jinsi ya kuhamisha mawasiliano WhatsApp kwenda Telegram

kwa sasa haya yanaweza kufanyika kwa watumiaji wa simu zinazotumia mfumo endeshi wa Android.

  • Ni baada ya minong’ono migi kuzuka kufuatia mabadiliko ya sera mpya ya faragha ya WhatsApp.
  • Kwa hatua tano tu, unaweza kuhamisha ‘chat’ zako na rafiki au ndugu yako kuelekea Telegram.
  • Telegram imefikia adhma hiyo baada ya kupata wahamiaji wengi ndani ya mwezi mmoja.

Dar es Salaam. Tangu WhatsApp itangaze sera mpya ya faragha inayotegemewa kufanya kazi  mwezi Mei mwaka huu, kumekuwa na minong’ono kutoka kwa watumiaji wake juu ya faragha ya mawasiliano wanayoyafanya katika tandao huo. 

Sera hiyo inayotarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapo Mei15, kinyume na tamko lililotolewa na watengenezaji wa mifumo wa mtandao wa Facebook wakati mtandao huo ulivyokuwa ukiinunua WhatsApp mwaka 2014 ambapo waliahidi kutokuhamisha taarifa (data) zozote za watumiaji wake.

Sehemu ya sera hiyo inaeleza kuwa, taarifa za watumiaji wa WhatsApp zitatumika na Facebook ambayo pia inamiliki mtandoa wa Instagram. 

Sintofahamu hiyo juu ya sera mpya ya WhatsApp imezua mjadala mpana kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii duniani huku wengine wakianza kutafuta mitandao mbadala itakayolinda faragha zao.

Mathalan, mtandao wa Telegram ambao kwa Januari pekee umepata watumiaji wapya milioni 100 umesema ongezeko hilo linachangiwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kutafuta “faragha na uhuru wa mawasiliano”Sehemu ya sera hiyo inaeleza kuwa, taarifa za watumiaji wa WhatsApp zitatumika na Facebook ambayo pia inamiliki mtandoa wa Instagram. Picha| Mtandao.

Taarifa iliyoandikwa katika tovuti ya Telegram inaeleza kuwa, licha ya kuwa watu wanahamia mtandaoni humo, bado kumbukumbu nyingi zikiwemo meseji, picha na video zinabaki katika mitandao ya kijamii waliyotokea ukiwemo mtandao wa WhatsApp. 

Kwa kuzingatia hali hiyo, mtandao wa Telegram umewezesha watumiaji wake wanaotumia simu janja zinazoendeshwa kwa mfumo endeshi wa Android kuhamisha chati zao kutoka WhatsApp hadi mtandaoni humo.

Kufanya hivyo, hizi ndizo hatua unazoweza kuzifuata ili kuhamisha chati zako kuelekea Telegram.

Ukiingia katika mtando wako wa WhatsApp, utabofya chati unayohitaji kuihamisha na kisha itaingia katika “chatroom” yako na rafiki, ndugu na kadhalika. Baada ya hapo, utabonyeza vitufe vitatu (options) vilivyopo upande wa kulia juu ya skrini yako.

Baada ya hapo utabonyeza zaidi (more) na kisha utabonyeza sehemu iliyoandikwa “export chat” na kisha utabonyeza app ya Telegram kama sehemu unayotaka kupeleka chati yako. Baada ya sekunde kadhaa, chati yako ya WhatsApp itahamia Telegram kama ilivyo.


Soma zaidi:


Mtaalamu wa programu tumishi na mifumo ya kidijitali, Emmanuel Evans amesema walichofanya WhatsApp kuleta sera mpya hakikuwa kitu kizuri kwani kila mtu ana haki na faragha ya mazungumzo au mawasiliano yake. 

“Ni heri wangelifanya kama Google wanavyofanya. Google wanakuuliza kama utahitaji takwimu zako wazitumie au laa,” amesema Evans.

Kwa upande wa Telegram, mtaalamu huyo amesema sera yake ya faragha iko sawa kwake kwani mtandao huo unahifadhi taarifa za watumiaji wake katika vituo vyao vya taarifa (data centre) na zinakuwa zimefichwa (encrypted).

“Kwangu mimi binafsi Telegram iko sawa,” amesema mtaalamu huyo.