October 7, 2024

Jinsi ya kuifunga akaunti yako ya Instagram kwa muda

Uzuri ni kwamba, akaunti yako itabaki kwenye kificho kwa muda wote utakaokuwa umeipumzisha na unaweza kuipata pale utakapoihitaji.

  • Hakikisha unakumbuka nenosiri na jina lako (user name) kabla ya kufuta akaunti yako.
  • Hatua hii inaweza kuwa faida kwa wale wanaotaka kuweka umakini kwenye mambo mengine na kuondokana na uteja wa mitandao ya kijamii.

Dar es Salaam. Mitandao ya kijamii inaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi katika maisha yako kama hautaidhibiti wakati wa kutumia ili kupata muda wa kufanya shughuli za maendeleo. 

Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu ambao unataka kujiweka kando na mtandao wa Instagram kwa muda, zipo dondoo zinazoweza kukusaidia kuifunga akaunti yako.

Nukta (www.nukta.co.tz) inakuletea hatua kwa hatua jinsi ya kuipumzisha (disable) akaunti yako ya Instagram endapo utahitaji kujielekeza katika shughuli nyingine.

Uzuri ni kwamba, akaunti yako itabaki kwenye kificho kwa muda wote utakaokuwa umeipumzisha na unaweza kuipata pale utakapoihitaji. 

Hata hivyo, utahitaji kukumbuka neno la siri na jina (user name) au anuani ya barua pepe kabla ya kuifunga akaunti yako. 

Tazama video hii kupata uelewa zaidi.