October 7, 2024

Tik Tok yafungua fursa ya matangazo kwa wafanyabiashara

Tiktok imesema matangazo ya bidhaa na huduma yataonekana kwenye ukurasa wa kwanza pale mtu anapoifungua programu ya Tik Tok.

  • Ni mpango wa kuwasaidia wafanyabiashara kuwafikia watu wengi kwa kutangaza kupitia mtandao huo. 
  • Mtoa matangazo anaweza kuweka tangazo lake kwenye mtandao huo na likaonekana mara tu mtu anapofungua app ya Tik Tok.
  • Kima cha chini cha matangazo ni Sh40,000 huku kampeni zikihitaji zaidi ya Sh155,000.

Dar es Salaam. Kama una mpango wa kujitanua katika biashara yako ya mtandaoni, mtandao wa Tik Tok umefungua jukwaa jipya kwa wafanyabiashara kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa.

Jukwaa hilo la Tik Tok for Business ni kama linalotumiwa na watumiaji wa WhatsApp Business na Instagram Business ambayo yote kwa pamoja yanalenga kuwawezesha wafanyabiashara kuwafikia wateja wengi zaidi wakiwa mtandaoni. 

“Haijalishi ukubwa wala udogo wa biashara yako, haijalishi ni kipi unatengeneza au kuuza, tunaamini “brand” yako inastahili kugunduliwa hapa (Tik Tok),” imeeleza TikTok katika taarifa yake ya uzinduzi wa huduma hiyo.  

Tiktok imesema matangazo ya bidhaa na huduma yataonekana kwenye ukurasa wa kwanza pale mtu anapoifungua programu ya Tik Tok.

Pia wataweza kuandaa mifumo ya kupiga kura za kimtandao (polls) na kuchangamana na wateja wao. Picha| Business news daily.

Pia watumiaji wa huduma hiyo watapata fursa ya mashindano ya “Hashtag”, video zinazochezwa kwa sekunde 3-5 (Brand Takeover),  na In-Feed Videos ambazo ni video zinazochezwa kwa urefu wa dakika moja zikiwa na sauti.

Kupitia mtandao huo, watoa matangazo wanaweza kuanzisha mashindano ya “Hashtag” ambayo yatawasiaidia katika kufikia watu wengi zaidi.

Pia wataweza kuandaa mifumo ya kupiga kura za kimtandao (polls) na kuchangamana na wateja wao.

Hata hivyo, Tik Tok haijaweka bayana mifumo ya bei za matangazo hayo lakini imesema bei itategemeana na kile kampuni (brand) inataka kupata.


Zinazohusiana


Mtandao huo  umesema kiwango cha chini cha matangazo ya kampeni ni zaidi ya Sh115,750 huku anayetaka kutangaza atakuwa na uwezo wa kuchagua kama matangazo hayo ni ya muda mfupi au muda mrefu.

Pia kwa matangazo ya kawaida, kima cha chini ni Sh46,300 ikiwa ni kwa matangazo ya muda mrefu na hata ya muda mfupi ambapo unaweza kuifanya pesa hiyo ikutangazie bidhaa na kampuni kwa muda utakaoupanga.

Tik Tok ni mtandao wa kijamii unaoruhusu kupakia picha na video za muda mfupi yakiwa na lengo la kuburudisha, kuelimisha na hata kukosoa.

Kati ya video ambayo imewafikia watu wengi zaidi ni pamoja na mashindano ya #DontRushChallenge ambayo imetamba wakati baadhi ya nchi zikilazimisha watu kubaki nyumbani kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona (Lockdown).