October 7, 2024

Corona yashusha bei magari yanayotumia umeme

Kampuni ya Tesla inayotengeneza magari ya umeme imesema itapunguza bei ya baadhi ya magari hayo ili kuvutiwa wateja wengi kwa sababu mahitaji yameanza kushuka kutokana na athari za janga la Corona.

  • Kampuni inayotengeneza magari hayo ya Tesla imesema itashusha bei ili kuvutia wateja wengi zaidi.
  • Imesema janga la Corona limeathiri manunuzi ya magari hayo. 

Kampuni ya Tesla inayotengeneza magari ya umeme imesema itapunguza bei ya baadhi ya magari hayo ili kuvutiwa wateja wengi kwa sababu mahitaji yameanza kushuka kutokana na athari za janga la Corona. 

Kampuni hiyo imesema punguzo hilo la bei litazifaidisha nchi za China na zile za bara la Amerika Kaskazini kwa magari aina ya Model 3, S na X n alitakuwa kati ya asilimia 4 hadi asilimia 6. 

Tesla imeeleza katika taarifa yake kuwa athari za janga la Corona limechangia kuongezeka kwa ukosefu wa ajira na kuathiri kipato cha watu wengi duniani, hivyo wameamua kupunguza bei ya magari ili kuvutia wateja.


Zinazohusiana:


Tesla inategemea kuuza magari 500,000 yanayotumia umeme mwaka huu lakini itategemeana mwenendo wa uchumi wa dunia ambao umeathiriwa na Corona. 

Magari ya umeme yamekuwa yakipigiwa chepuo na watetezi wa mazingira kwa sababu ni njia mojawapo ya kulinda mazingira hasa kupunguza uchafuzi wa hewa.