November 24, 2024

Jinsi ya kuwa na mwonekano mzuri wakati ukiwasiliana kwa njia ya video

Picha hizo (Virtual backgounds) zinaweza kutumika kama mbadala wa sehemu ya nyuma ya sura yako na ukaonekana vizuri na watu wanaokutazama wakati mkiongea kwa kutumia video.

  • Kwa wanaotumia Zoom unaweza kubadilisha sehemu ya nyuma kwa kuweka picha unayotaka.
  • Pia matumizi ya programu ya ChromaCam yanaweza kukusaidia. 

Dar es Salaam. Ni dhahiri kuwa kwa sasa teknolojia ya video inayotumika kuwasiliana mtandaoni imeshamiri kila mahali. Hiyo inatokana na ukweli kuwa watu wengi wanafanyia kazi nyumba na ili kuhakikisha kila kitu kiko juu ya mstari wanatakiwa kuwasiliana kwa njia ya video (Video teleconferencing).

Baadhi ya programu maarufu (Apps) zinazotoa huduma hiyo ni pamoja na Zoom, Google Meet na WebEx Teams. 

Licha ya uzuri wa programu hizo katika kuwasiliana, changamoto inabaki muonekano wa eneo unaloonekana wakati wa mawasiliano ya video hasa sehemu ya nyuma ya sura yako (background). 

Sehemu hiyo ya nyuma kwa baadhi ya watu huwaletea mawazo au kukosa utulivu na hivyo mtu hujitahidi kutafuta eneo zuri atakalotumia wakati wa mawasiliano ya video. 

Hata hivyo, kwa watu ambao hawaridhishwi au hawapendi maeneo yao yaonekane kwenye video, teknolojia inaweza kufanyia kitu kwa kuwatafutia picha nzuri ambazo wanaweza kuzitumia. 

Picha hizo (Virtual backgounds) zinaweza kutumika kama mbadala wa sehemu ya nyuma ya sura yako na ukaonekana vizuri na watu wanaokutazama wakati mkiongea kwa kutumia video. 


Zinazohusiana: 


Kwa wanaotumia Zoom, ni rahisi sana.  Fungua programu ya Zoom kwenye kompyuta yako kisha gusa sehemu “settings” ambayo utaikuta upande wa kulia juu.

Baada ya hapo, chagua “Virtual Background”. Hapo utakutana na picha mbalimbali ambazo Zoom wamekuwekea. Chagua moja unayoipenda ili itumike nyuma yako wakati ukiongea kwenye video. 

Zoom inakuwezesha kupata picha mbalimbali utakazotumia wakati wa mawasiliano ya video. Picha| Todd Haselton.

Lakini Zoom, inakupata uchaguzi wa kutumia picha zako binafsi ambazo umehifadhi kwenye kompyuta. Kama kawaida gusa sehemu ya “settings” bonyesha kitufe cha “+” ambacho kitakupeleka mpaka kwenye kompyuta yako na kisha utaingiza picha unayopenda. 

Zoezi hilo unaweza kulifanya hata kama unatumia simu ya mkononi kwa kufuata maelekezo hapo juu. 

Kwa wale wanaotumia Google Meet na WebEx Teams hawana kipengele cha kubadilisha sehemu ya nyuma bali unaweza kutumia programu maalum. 

Programu hiyo ya ChromaCam unaipakua kwenye simu au kompyuta ambayo ina picha nzuri ambazo wakati unatumia Google Meet au WebEx Teams unaweza kuiunganisha na ikakuwekea picha nzuri nyuma yako. 

App ya ChromaCam inaweza kubadilisha sehemu ya nyuma na ikafanya kuwa na mwonekano mzuri. Picha| ChromaCam.