October 6, 2024

Airbnb yatoa masharti mapya kwa wapangishaji nyumba

Kampuni hiyo yenye makao makuu yake nchini Marekani imesema kuwa kuanzia Mei mwaka huu, wapangishaji wanatakiwa kuimarisha usafi katika nyumba wanazopangisha ili kuwakinga wateja wao na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).

Baadhi ya hoteli na nyumba za kulala wageni zimefungwa kipindi hiki kuepuka Corona. Picha|Mtandao.


  • Ni pamoja na kuacha nyumba wazi  kwa saa 24 kabla hajaruhusiwa kuingia mgeni mpya.
  • Dhamira kuu ya taratibu hizo ni kuondoa uwezekano wa maambukizi ya virusi vya Corona hata baada ya shughuli za kitalii kuendelea.
  • Watakaoendana na masharti hayo kupewa uthibitisho na mpangaji anaweza kuona wakati anatafuta nyumba ya kupanga.

Dar es Salaam. Kampuni inayoratibu upangishaji nyumba mtandaoni ya Airbnb imetangaza masharti mapya kwa wapangishaji wanaotumia huduma zake ikiwemo kuacha nyumba wazi kwa saa 24 kabla hajaruhusiwa kuingia mteja mpya. 

Kampuni hiyo yenye makao makuu yake nchini Marekani imesema kuwa kuanzia Mei mwaka huu, wapangishaji wanatakiwa kuimarisha usafi katika nyumba wanazopangisha ili kuwakinga wateja wao na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) 

Nyumba itatakiwa kuachwa wazi kwa saa 24 kabla ya kumpangisha mtu mwingine.

Kwa mujibu wa Airbnb, kiwango hicho ni cha kwanza kufikiwa ikiwa ni kati ya mapendekezo yalitotolewa na Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC)

Airbnb imefikia hatua hiyo ikiwa ni adhimio la kupunguza maambukizi yakiwemo ya virusi vya Corona baada ya nchi mbalimbali kuanza kulegeza masharti ya kukaa ndani na kurusu shughuli za uchumi. 

“Ifikapo Mei, tutazindua taratibu mpya zenye maboresho juu ya kusafisha kila chumba kwenye nyumba. Taratibu hizo zitaambatana na mafunzo na uthibitishaji kwa wapangishaji,” imesomeka taarifa ya Airbnb.


Zinazohusiana


Zaidi, ifikapo Mei kampuni hiyo inayoshika kasi kwenye shughuli za utalii imesema mtu anayetaka kupanga ataweza kuona nyumba ambazo zimethibitishwa kupata mafunzo hayo.

Licha ya kuwa wageni wengi wanaridhishwa na usafi wa nyumba wanazopanga kiasi cha kufikia asilimia 94 ya wageni hao kuisifu kwa nyota tano na nne, bado kampuni hiyo imeona haja ya kuendelea kufanya maboresho hayo ili kuruhusu mzunguko wa hewa na usafi timilifu kwenye chumba kambla mtu mwingine hajaingia.

Taratibu hizo zitaenda sambamba na taarifa maalumu kuhusu tahadhari dhidi ya virusi vya corona ikiwemo matumizi ya dhana za kujikinga zikiwemo barakoa na vikinga mikono (gloves).

Taratibu hizo zitahitajika kufuatwa na kila mpangishaji na kwa ambaye hatoweza kuacha nafasi baina ya mtu na mtu (saa 24) huduma zake zitafungwa saa 72. 

Hatua hizo zitasaidia kuwakinga watu hasa watalii wanaokuja nchini kupanga nyumba kwa kutumia programu hiyo kujilinda dhidi ya Corona.