October 8, 2024

Mbinu zitakazokuepusha na Corona ukiwa kwenye gari

Wakati huu ambao huwezi kumbaini mgonjwa wa virusi hivyo kwa kumtazama, haya ni mambo ambayo unaweza kuzingatia ili kuwa salama na kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo wakati ukitumia gari lako

  • Tumia vitakasa vilivyoidhinishwa kimataifa.
  • Pendelea kuosha gari yako mwenyewe na hakikisha hautumii maji mengi.
  • Hakikisha haukosi vitu muhimu vikiwemo vitakasa mikono na barakoa kwenye gari yako.

Dar es Salaam. Huenda unajihisi upo salama kwa kuwa hautumii usafiri wa umma lakini vipi kuhusu gari lako? Bado unatakiwa kuchukua tahadhari.

Wakati huu ambao huwezi kumbaini mgonjwa wa virusi hivyo kwa kumtazama, haya ni mambo ambayo unaweza kuzingatia ili kuwa salama na kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo wakati ukitumia gari lako:

1. Tumia vitakasa vyenye kemikali ya “Hydrogen peroxide” ambayo haitadhuru baadhi ya sehemu za gari lako. Unaweza kuipata kwenye duka la dawa na kisha kuiweka kwenye chombo cha kupulizia. 

Kusafisha unaweza kupulizia kemikali hiyo sehemu mbalimbali za gari na kisha kufuta na kitambaa kisafi. 

Hakikisha unakifua kitambaa hicho kwa sabuni baada ya kutumia na unashauliwa kutumia vikinga mikono (gloves) wakati unafanya shughuli hizo.

2. Pendelea kuosha gari lako mwenyewe wakati huu wa mlipuko wa Corona. Hii itakusaidia gari yako kutokugusa hasa ndani na watu ambao huwafahamu.

Pendelea kuosha gari lako kwani huwezi kujua kama anayekufanyia kazi hiyo yupo salama.  Picha| Giphy.

Ni muhimu kuchukua tahadhari zote kipindi hiki ili kulifanya gari lako kuwa mahali salama na kuepuka maambukizi.

3. Hakikisha hukosi vifaa vya kujikinga vikiwemo barakoa na vitakasa vya kujisafisha mwenyewe na kushafisha gari lako. 

Unaweza kununua barakoa na kuvaa baada ya kushuka kwenye gari lako na kuelekea mahala penye watu wengi kama sokoni na maeneo mengine.

Pia unaweza kuhakikisha unakuwa na visafishio vya vioo vya gari vyenye vitakasa (wipes) zilizoidhinishwa kwa kiwango cha kimataifa kwani siyo kila kitakasa kinaweza kukukinga na virusi vya Corona.


Zinazohusiana


4. Ni vizuri kutumia dhana hizo kwa kiasi kwani endapo utatumia kwa zaidi, huenda unyevu akaobaki ukakuletea harufu isiyopendeza kwenye gari lako na hata kusababisha fangasi kuzaliana. Tumia kiasi tu.

Kama unafahamu njia nyingine ya kuwasaidia wadau wanaotumia usafiri binafsi, usiache kuacha maoni yako kwenye kurasa zetu za mitandao ya  kijamii.