Mambo ambayo kila mwenye gari anapaswa kuyazingatia
Kwa kuyafahamu mambo haya ambayo mara nyingi huonekana ni madogo, itakuepusha na gharama amabazo siyo za msingi na hueda pesa hiyo ungeifanyia mambo mengine ya maana.
- Epuka gharama za ziada kwa kubadilisha oili ya injini yako kwa muda uliopangwa.
- Hauna sababu ya kununua matairi mapya kila mara, badilisha tairi lako la mbele na uliweke nyuma ili yadumu kwa muda mrefu.
- Badilisha vichuja hewa vyako kwa muda uliopangwa la sivyo, kiyoyozi kipya kinakuhusu.
Dar es Salaam. Huenda umekuwa ukiingia gharama kubwa wakati ukitumia gari lako kwa makosa ambayo yanaweza kuzuilika.
Kati ya mambo hayo madogo madogo, moja wapo linaweza kuwa kupitiliza muda wa matengenezo ya vifaa vya gari lako kama inavypendekezwa na mtoa huduma wako.
Lakini bado una nafasi nzuri ya kulifanya gari lako lidumu muda mrefu kwa kufahamu baadhi ya mambo ambayo huenda hukuwa unayawekea uzito wakati ukitumia gari lako kwa shughuli mbalimbali.
Kwa kuyafahamu mambo haya ambayo mara nyingi huonekana ni madogo, itakuepusha na gharama ambazo siyo za msingi na pesa yako ukaielekeza katika mambo mengine:
Hakikisha una taili la akiba
Mara nyingi watu huliona hili kama jambo la muhimu pale wakiwa na safari ndefu. Lakini mtanange unakuja pale dharura inapotokea.
Ukipata dharura njiani itakulazimu kununua tairi jipya au kutafuta msaada wa watu wakusaidie kupata tairi lingine, jambo litakalokusababishia usumbufu mkubwa na pesa zinaweza kukutoka.
Kwanini uingie gharama hizi na kupoteza muda wako wakati unaweza ukawa na taili lako kwenye gari? Fanya maamuzi na jifunze jinsi ya kufunga taili kwenye gari yako.
Pia unashauriwa kubadilisha mataili yako pale linapokuwa limeisha ili kuepuka ajali. Kwa mujibu wa tovuti ya daveramsey.com, unashauriwa kubadilisha matairi ya mbele ya gari na kuyaweka nyuma kwani kila tairi huisha kwa namna yake.
Taili za mbele na za nyuma huisha kwa tofauti hivyo chukua muda ubadilishe mataili yako. Itasaidia mataili yako kudumu kwa muda mrefu kwani hayatoisha upande mmoja au ule upande ambao huanza kuisha kila mara.
Unachagua kipi? Kubadilisha oili au injini? Akili kichwani mwako. Picha| Huntington.
2. Badilisha oili ya gari
Unafikiri haiwezi kukuingiza kwenye gharama? Hakika unajidanganya! Kwa kawaida, inashauriwa kubadilisha oili yako kila baada ya kutembea kilometa 8046.7 au miezi sita japo inatofautiana gari moja hadi jingine.
Fundi wa magari katika duka la vifaa vya magari la Bonny’s Sound jijini Dar es Salaam, Samuel Ng’ambi amesema inagharimu takriban Sh65,000 kuweka oili mpya kwenye gari lakini mtu asipobadilisha kwa wakati, injini ya gari yake inaweza kupata matatizo na kuingia gharama kubwa za matengenezo.
Unachagua kipi? Kubadilisha oili au injini? Akili kichwani mwako.
Zinazohusiana
- Wanafunzi wa NIT waja na gari la umeme kama Tesla
- Hivi ndivyo gesi asilia inavyopunguza ukali wa maisha kwa wamiliki wa magari
- Namna wenye magari ya gesi asilia wanavyookoa maelfu ya fedha Tanzania
2. Badilisha vichuja hewa vya gari
Vinajulikana kwa “airfilter” ambavyo kazi yake ni kuchuja hewa inayoingia na kutoka nje ya gari
Ng’ambi amesema kushindwa kubadili vifaa hivi kutakupelekea kuongeza gesi ya kiyoyozi chako pamoja na kubadili vichuja hewa vya gari na hivyo kufanya gharama kuzidi kuwa kubwa.
Kwanini uingie gharama ya kubadili vitu viwili huku unaweza kubadili kimoja na ukaokoa gharama. Acha kuchukulia mambo poa.
Ungependa tukujuze nini katika kona hii ya teknolojia? Tufikie kupitia mitandao yetu ya kijamii.