November 24, 2024

Google sasa kukuchagulia usafiri wa ndege wa bei nafuu

Watu wanaotaka usafiri wa bei chee nao kuhudumiwa kama ilivyo kwa wenye fedha nyingi.

  • Ni mfumo unaohusisha kutoa usafiri kulingana na bajeti ya mtu.
  • Umuhimu wa mfumo huu ni kwamba unampatia mtu usafiri huo kwa kufuata uwezo wake wa kifedha. 
  • Watu wanaotaka usafiri wa bei chee nao kuhudumiwa kama ilivyo kwa wenye fedha nyingi. 

Huenda unapanga kusafiri au kutembelea nchi mbalimbali mwishoni mwa mwaka huu na unatarajia kutumia usafiri wa ndege. 

Kampuni ya teknoolojia ya Marekani ya Google imetengeneza mazingira mazuri ya mtu kutafuta usafiri wa ndege kuendana na bajeti aliyoiweka kwa ajili ya safari aliyopanga kufanya kwa muda maalum.

Kupitia Google Flights, mtu ana uwezo wa kuweka taarifa za mahali anapotarajia kutembelea na gharama alizopanga kutumia ili kufanikisha safari yake, kwa ndege itakayopatikana inayoendana na taarifa alizoingiza.

Kwa kuingiza taarifa za mahali unapotaka kutembelea, tarehe ulizopanga kusafiri na bajeti uliyonayo, mfumo una uwezo wa kuleta usafiri wa ndege unaoendana na taarifa ulizoingiza katika programu tumishi hiyo. 

Taarifa utakazopata zitakupa uwezo wa kufanya maamuzi ya kama usafiri huo utakufaa katika safari unayotarajia kuifanya. 

Umuhimu wa mfumo huu ni kwamba unampatia mtu fursa ya kupata usafiri wa ndege kutokana na uwezo wa kifedha alionao. 


Zinazohusiana:


Teknolojia ya kutafuta usafiri wa ndege kwa kutumia programu tumishi ni maarufu, lakini uwezo wa mifumo hiyo kuchuja taarifa za mteja na kumpatia usafiri kulingana na uwezo wake ni ubunifu na ni teknolojia iliyoanzishwa na Google flights kwa mara ya kwanza.

Je, unafahamu programu tumishi nyingine zinazoweza kumsaidia mtu kupata huduma za usafiri wa ndege kutokana na kibubu chake? Tujulishe kupitia tmalopa@nukta.co.tz