October 6, 2024

Google Maps yawakumbuka tena watumiaji wa simu za Iphone

Safari imefungua mlango kwa watumiaji wa simu hizo kutumia bidhaa yake ya “Google Maps” iliyoboreshwa zaidi ambayo inawawezesha kujua hali ya barabara wakati wowote kwa kuwajulisha kama kuna ajali imetokea, barabara inajengwa au inafanyiwa ukarabati.

  • Inawawezesha kujua hali ya barabara wakati wowote kwa kuwajulisha kama kuna ajali imetokea, barabara inajengwa au imefungwa.
  • Mabadiliko haya yanasaidia watumiaji wa barabara kupata taarifa mapema kabla hawajapoteza mafuta na muda mwingi barabarani.
  • Huduma hiyo tayari inatumika katika simu za Android. 

Watumiaji wa simu za Iphone, sasa wana kila sababu ya kutabasamu kwa sababu kampuni ya Google inazidi kuwasogelea kila siku kwa huduma mbalimbali za teknolojia.

Safari imefungua mlango kwa watumiaji wa simu hizo kutumia bidhaa yake ya “Google Maps” iliyoboreshwa zaidi ambayo inawawezesha kujua hali ya barabara wakati wowote kwa kuwajulisha kama kuna ajali imetokea, barabara inajengwa au inafanyiwa ukarabati.

Pia inawasaidia watumiaji wa simu hizo zinazotumia programu endeshi ya iOS kujua kama barabara wanayotaka kutumia kama imefungwa na haitumiki kwa wakati husika. 

Huduma hiyo ambayo tayari ilianza kutumika kwa watumiaji wa simu za Android, inalenga kumrahisishia maisha mtumiaji wa barabara na kumpunguzia muda wa kukaa barabarani muda mrefu na gharama za mafuta.  


Zinazohusiana: 


Ili kupata taarifa ya barabara unayotaka kutumia, unapaswa kwenda Google Maps, kisha bonyeza kitufye chenye alama ya kuweka tukio jipya chini ya alama inayoonesha mwelekeo (compass direction) kisha ataweka taarifa yako ya unakokwenda.

Baada ya kuweka taarifa zako, utaletea taarifa zote za barabara husika ikiwemo hali ya foleni  kama ambavyo zimekuwa zikitolewa awali na picha halisi ya kizuizi cha barabarani kama ni ajali, ujenzi au barabara imefungwa.

Kwa sasa, mtumiaji wa Google Maps, anaweza kujua mwendo anaotakiwa kutembea akiwa barabarani kulingana na foleni na hali ya foleni katika barabara mbalimbali z aeneo lake.