October 6, 2024

Google Doc yawaboreshea huduma watumiaji wake

Iko mbioni kuongeza kipengele kipya kitakachomuwezesha mtumiaji kufahamu idadi ya maneno anayoandika kama ilivyo kwa wanaotumia pragramu ya Microsoft word.

  • Iko mbioni kuongeza kipengele kipya kitakachomuwezesha mtumiaji kufahamu idadi ya maneno anayoandika kama ilivyo kwa wanaotumia pragramu ya Microsoft word.
  • Itawasaidia watumiaji kufahamu ukomo wa maneno wanayoandika katika programu hiyo ambayo iko chini ya kampuni ya Google. 

Watumiaji wa huduma ya Google Doc kama sehemu ya kuandikia nyaraka mbalimbali, huenda wakapata ahueni baada ya kampuni ya Google kuiboresha huduma hiyo ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wake.

Mabadiliko hayo ni kuongezwa kwa kipengele kipya kitakachomuwezesha mtumiaji kufahamu idadi ya maneno anayoandika kama ilivyo kwa wanaotumia pragramu ya Microsoft word.

Kwa sasa watumiaji wa Google Doc wanaweza kuandika maandishi lakini hawawezi kuhebu idadi ya maneno waliyoandika, jambo ambalo limekuwa likiwapa changamoto hasa wanapotaka kuwa na idadi fulani ya maneno. 


Zinazohusiana:


Ili kujua idadi ya maneno unayoandika katika ukurasa unaondikia maandishi, utalazimika kwenda menu halafu katika kipengele cha vitendea kazi (Tools) halafu kwenye kuhesabu maneno (Word Count) ndipo mtu anapoweza kuanza kuona idadi ya maneno yaliyoandikwa katika kurasa wake.

Mabadiliko haya yataanza kutumika na watumiaji wa mtandao wa G suite ambao uko chini ya Google mwanzoni mwa mwezi Oktoba, ambapo watumiaji watakuwa na uhuru wa kuandika maandiko mbalimbali kwa idadi wanayoitaka.