October 6, 2024

Facebook yazigeukia Serikali za mitaa

Hivi karibuni, mtandao huo umezindua mfumo mpya (tool) ya mawasiliano utakaotumiwa na mamlaka za Serikali za mitaa duniani kuwasiliana na kutoa taarifa za maendeleo kwa wananchi wa maeneo yao kwa urahisi na haraka.

  • Ni baada ya kuanzisha mfumo wa “local alert” anaozisaidia Serikali za mitaa kutoa taarifa kwa urahisi na haraka kwa watu wake.
  • Pia unatumika wakati wa majanga kama moto na mafuriko yanayohitaji msaada wa haraka wa waokozi. 
  • Kwa sasa unatumika Marekani lakini unaweza kusambaa katika nchini nyingine hapo baadaye.

Dar es Salaam. Kwa muda mrefu sasa, mtandao wa Facebook umeendelea kujijenga na kuboresha huduma zake ili kuwapa kilicho bora watumiaji wake kulingana na mahitaji yao.  

Hivi karibuni, mtandao huo umezindua mfumo mpya (tool) ya mawasiliano utakaotumiwa na mamlaka za Serikali za mitaa duniani kuwasiliana na kutoa taarifa za maendeleo kwa wananchi wa maeneo yao kwa urahisi na haraka. 

Mfumo huo wa kidijitali ulianza kufanyiwa majaribio mwaka 2018, umeanza kutumika Marekani  lakini huenda ukafika katika  mataifa mengine ikiwemo Tanzania siku zijazo ili kuhakikisha taarifa za ofisi za Serikali za mitaa zinawafikia watu kwa muda muafaka.

Mfumo huo unaojulikana kama “local alert” unafanya kazi kwa urahisi ni kama mtu anapoweka picha yake na kuchagua nani aione na nani aisiione, mfumo huu unawezesha mamlaka kuchagua ujumbe huo uwe kwenye kipengele cha “local alert” ambapo kampuni ya facebook moja kwa moja itaufikisha ujumbe huo kwa watu wote wanaokaa kwenye jamii hiyo.

Mmoja kati ya watumiaji wa mtandao wa facebook huko Marekani ameshanufaika na matumizi ya mfumo huo baada ya kutumia taarifa za mafuriko.

“Licha ya watu kuwa karibu kimawasiliano, bado inakua ngumu kuwafikia watu wote nyakati za dharura. “Local Alerts” inasaidia kufikia watu wengi kwa kutumia ujumbe. 

“Ni mfumo mzuri unaosaidia kufikisha ujumbe kwa watu wanaouhitaji zaidi,” amesema Shane Reichardt ambaye anafanya kazi kwenye moja ya mamlaka ya dharura nchini Marekani.

Mfumo huo pia unasaidia kufikisha taarifa kwa haraka hasa zile zinahusu majanga kama moto na mafuriko ambazo zinahitaji msaada wa haraka wa mamlaka za uokozi.

Hadi sasa, mtandao wa Facebok umeanzisha mifumo mingi muhimu ikiwemo “Safety Check” ambao unamruhusu mtu kuwataarifu ndugu na rafiki kuwa yuko salama pindi yatokeapo majanga.


Zinazohusiana:


Kwa mujibu wa wadau wa mitandao ya kijamii, kama huduma hiyo itafika nchini basi itakua na msaada mkubwa na kusaidia kuzuia vifo na uharibifu wa mali usio wa lazima.

Meneja wa kampuni ya kusaga unga ya Lina mills ya jijini Dar es Salaam, Christian Kulwa amesema katika majanga ya moto, taarifa huchelewa kulifikia jeshi la zimamoto hivyo kufanya mali nyingi kuteketea baada ya majaribio ya kudhibiti moto huo kushindikana.

“Itakua msaada kwenye jamii za kitanzania kwani itasaidia watu kushirikiana kudhibiti majanga wakati wakisubiria wataalamu,” amesema Kulwa.

Hata hivyo, mfumo huo hautumiki na watu wote, usipokuwa mtu awe amesajiliwa kama Serikali ya mtaa au watu wanaofikiwa na taarifa za dharura kama polisi na jeshi la zimamoto.