Facebook kubadili mwelekeo wa makundi ya watumiaji wake
Yatasaidia kupunguza mrundikano wa jumbe zisizokua na matumizi katika mtandao huo.
- Yatasaidia kupunguza mrundikano wa jumbe zisizokua na matumizi katika mtandao huo.
- Pia watumiaji hawakua na uwezo tena wa kutuma meseji kama ilivyo sasa.
- Makundi hayo yatakua yanatumika zaidi kwenye App ya Messenger.
Mtandao wa kijamii wa Facebook unakusudia kuboresha huduma zake kuondoa utaratibu wa watumiaji wake kutumiana meseji kwenye makundi ya mtandao huo kwa lengo kurahisisha mawasiliano ya watumiaji wake na kuwaondolea usumbufu wa kuungwa kwenye makundi wasiyotaka.
Maboresho hayo yanatarajiwa kuanza kutumika Agosti 22 mwaka huu ambapo kila mtu alieunganishwa katika kundi lolote kwenye mtandao huo hatakua na uwezo wa kutuma meseji tena kama ilivyokua awali.
Kwa mujibu mtandao wa TechCrunch, utaratibu huo wa Facebook umeanzishwa kwa lengo la kuongeza njia za kuwasiliana kwa urahisi, baada ya kuona ongezeko la meseji zisizo na matumizi katika mtandao huo ili kuondoa kero zinazowakabili watumiaji wake.
Uwezekano wa mtu yeyote kumuunganisha mtu asiemjua katika kundi na kumtumia meseji umeongeza ukakasi uliowasukuma wataalam kuondoa kipengele hicho katika mtandao.
Zinazohusiana:
- Facebook yaja na tovuti ya ‘usiri’ kuwasaidia wafanyabiashara kuelewa sera zake
- Facebook yafanya maboresho utafutaji wa bidhaa mtandaoni.
Facebook haijatoa tamko rasmi la mabadiliko hayo yatakayofanyika siku mbili zijazo bali watumiaji wote watakaokua wanatumia makundi wanaweza kujikuta nje ya makundi au kukosa uwezo wa kuandika chochote katika makundi waliokuanayo hapo awali.
Hata hivyo, mabadiliko haya hayataathiri utendaji kazi wa programu tumishi (App) ya Facebook ya Messanger, kwa sababu makundi yaliopo kwenye App hiyo yataendelea kutumika isipokua yale yaliyopo Facebook ndiyo hayatakua yanafanya kazi tena kwa mujibu wa tetesi za wachambuzi wa masuala ya mitandao ya kijamii.
Pia, bado haijawa bayana iwapo mabadiliko hayo yataathiri makundi ambayo mtumiaji kaomba kujiunga ama la.