October 7, 2024

Facebook yawarahisishia maisha wapenzi wa filamu

Inakusudia kuwawekea kipengele cha kupata taarifa za filamu wanazozipenda kwa urahisi na haraka.

  • Inakusudia kuwawekea kipengele cha kupata taarifa za filamu wanazozipenda kwa urahisi na haraka.
  • Pia itawawezesha kupata tiketi na kufahamu kumbi za sinema zinazoonyesha filamu husika. 

Katika kuwafikia na kukidhi mahitaji ya watumiaji wake, Facebook iko mbioni kuanzisha kipengele kipya kitakachowarahisishia wapenzi wa filamu kupata kwa haraka risiti zinazowawezesha kuingia katika kumbi za sinema. 

Kipengele hicho kinatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni ambapo mpenzi wa filamu ataweza kutafuta filamu anazizopenda na kujulishwa pale filamu hiyo inapokua imetoka kwajili ya kutazamwa.

Mteja atatakiwa kuingia katika ukurasa wake wa juu (News feed) na kuchagua filamu anayoipenda na kubonyeza kitufe cha  ‘Interested’ CTA button’ kitakachomwezesha kupata taarifa zote pindi filamu hiyo inapokua iko tayari.


Zinazohusiana


Mabadiliko mengine ni pamoja na mtumiaji ataweza kutafuta filamu anayopenda katika “Search Engine” na kupata taarifa za kina kuhusu filamu hiyo ikiwemo namna ya kupata tiketi na ukumbi anaoweza kuipata filamu hiyo.

Mabadiliko haya yataleta urahisi kwa wapenzi wa filamu kujua ni filamu gani zimetoka karibuni na kufuata taratibu zote zinazotakiwa kufanyika kwa urahisi bila kupata shida yoyote kama ambavyo mtu angekua akifanya bila ya maboresho hayo kufanyika hapo awali.