Twitter kuwawekea watumiaji wake kipengele cha kupanga picha kwa mtiririko wanaoutaka
Kipengele hicho kiko kwenye majaribio na kikamilika kitawapa uhuru zaidi watumiaji wa mtandao huo kupanga picha watakavyo.
- Kipengele hicho kiko kwenye majaribio na kikamilika kitawapa uhuru zaidi watumiaji wa mtandao huo.
- Itakuwa ahabari njema kwa watu wanaopenda kupanga picha kwa mtiririko wanaoutaka katika mabandiko yao.
Hatimaye changamoto wanayoipata watumiaji wa mtandao wa Twitter ya kupanga picha watakavyo katika mabandiko (post) Yao itafika mwisho, baada ya suluhisho kupatikana.
Kwa mujibu wa ugunduzi uliofanywa na Mtaalam wa kujitegemea wa masuala ya mitandao ya kijamii, Jane Manchun Wong, Twitter inafanyia kazi kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtu kupanga picha kwa mtiririko anaoutaka kwa kutumia mchakato rahisi wa ‘drag and drop’.
Huenda hiyo itakua habari njema kwa watumiaji wa mtandao huo, ikizingatiwa kwa sasa hawezi kupanga picha katika mtiririko wanaoutaka wakati wanaweka ujumbe Twitter.
Twitter will let users drag to reorder photos while composing a tweet pic.twitter.com/rgcbIk9IqB
— Jane Manchun Wong (@wongmjane) July 25, 2019
Mabadiliko hayo ni madogo lakini yana maana kubwa kwa watumiaji ambao wanapenda kuwa na machaguo mbalimbali wakati wakitumia mtandao huo. Pia itaondoa usumbufu wa kufuta na kuweka picha ili zikae kama mfumo wa Twitter unavyotaka.
Hata hivyo, Twitter bado hawajazungumza neno lolote kuhusu mabadiliko hayo, lakini yatakapokamilika na kuanza kutumika yatakua ni habari njema kwa watumiaji wa mtandao huo unaokua kwa kasi duniani.