November 24, 2024

Apple yatangaza kuzifanyia marekebisho simu za Iphone 6S

Kampuni ya simu ya Apple imetangaza kutoa ofa ya kutengeneza bure simu aina ya Iphone 6S na 6S Plus ikiwa zitapata matatizo ya kuzimika ghafla wakati wa kuzitumia.

  • Imetangaza hatua hiyo, baada ya kubaini baadhi ya simu hizo zina changamoto ya kuzimika ghafla.
  • Simu hizo ni zile zilizotengenezwa kati ya Agosti 2018 na Oktoba mwaka huu.

Kampuni ya simu ya Apple imetangaza kutoa ofa ya kutengeneza bure simu aina ya Iphone 6S na 6S Plus ikiwa zitapata matatizo ya kuzimika ghafla wakati wa kuzitumia. 

Huduma hiyo itawahusu watumiaji wa Iphone  walionunua simu hizo kati ya Agosti 2018 na Oktoba mwaka huu, baada ya kampuni hiyo ya Marekani kubaini kuwa moja ya kifaa cha simu hizo hakiko sawa. 

Hali hiyo imeiweka Apple katika tahadhari ya lolote linaloweza kutokea kwa wateja wa simu hizo na jinsi wanavyoweza kuwasaidia kutatua changamoto hiyo inayoweza kutokea ikiwemo kufanya matengenezo na kuweka kifaa kipya kupitia programu maalum.  

Ili kupata huduma hiyo, mteja atatakiwa kufuata utaratibu maalum unaopatikana kwenye tovuti ya kampuni hiyo, kisha kuingiza namba ya simu (Serial number) ili kuangalia kama simu yake ni moja ya simu inayohitaji huduma hiyo na kufuata maelekezo mengine yanayofuata.


Zinazohusiana: 


Pia mhusika anaweza kupata huduma hiyo ya matengenezo kwa wakala anaetambulika na Apple, kuweka miadi katika duka lolote linalouza vifaa vya rejareja la iOS. 

Kampuni hiyo imetoa angalizo kuwa matengenezo yoyote yatakayoongezeka zaidi ya tatizo hilo yatakuwa ndani ya gharama za mtu binafsi na siyo kampuni.

Hata hivyo, Apple hawajatoa taarifa zaidi juu ya sehemu yenye tatizo na kitu kinachosababisha simu hiyo kuwa na tatizo hilo.