October 7, 2024

Facebook waja na hiki kwa watumiaji wenye wafuasi wengi

Mtandao huo wa kijamii wa Facebook umeanzisha kipengele cha kuwatumia ujumbe marafiki wa karibu (Top pages) ili kumwezesha mtumiaji wake kuwasiliana kwa ukaribu na marafiki zake.

Dar es Salaam. Mtandao wa kijamii wa Facebook umeanzisha kipengele cha kuwatumia ujumbe marafiki wa karibu (Top pages) ili kumwezesha mtumiaji wake kuwasiliana kwa ukaribu na marafiki zake.

Kipengele hicho kinaweza kuwa ni moja ya huduma za kuvutia kwa watumiaji wa mtandao huo ulimwenguni ambao kwa sasa unakadiriwa kuwa na watumiaji bilioni 2. 

Hata hivyo, siyo kila mtumiaji wa Facebook atanufaika na huduma hiyo.

Watumiaji wa Facebook watakaonufaika na kipengele hicho ni wale ambao wana wafuasi kuanzia 10,000 (10k followers) huku sifa nyingine ukihitajika kuwa na umri kuanzia miaka 28.

Kupitia kipengele hicho mtumiaji wa Facebook ataweza kuwashukuru  mashabiki wake maarufu au kuwatumia habari za kipekee ambazo wafuasi wake wengine hawataweza kuzipata.

Mabadiliko hayo tayari yameanza kuonekana kwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ulimwenguni kuanzia mwezi uliopita huku ikitarajiwa kuwafikia watu wengine wakati wowote.

Kipengele hicho kinachohusisha mashabiki  wa karibu (Top Fans) kinaweza kuwa ni fursa nyingine kwa mtumiaji wa Facebook kuweza kujenga mahusiano bora na marifiki zao wa karibu katika jamii wanazoishi.

Hii ni moja ya huduma za hivi karibuni katika uboreshaji wa mtandao huo ambao unakabiriwa na ushindani mkubwa kutoka katika mitandao mingine ikiwemo Twitter.