Facebook yaanza mchakato wa kufuta makundi ya watumiaji wake
Kuanzia Septemba 26, watumiaji wake hawataweza kuweka picha kwenye kipengele cha stori (story section) katika makundi ya mtandao huo.
- Kuanzia Septemba 26, watumiaji wake hawataweza kuweka picha kwenye kipengele cha stori (story section) katika makundi ya mtandao huo.
- Badala yake anaweza kutumia namna nyingine ya kuiweka picha hiyo kwa njia ya kawaida ndani ya kundi.
- Wadau wasema hiyo ni hatua ya mwanza kwa facebook kuyafuta kabisa makundi ya watumiaji.
Dar Es Salaam. Katika safari yake ya kufuta makundi ya Facebook, mtandao huo sasa wamekusudia kufuta picha zote zilizopo kwenye sehemu ya stori (Story section) na hataruhusu tena watumiaji wake kuweka stori hizo kwenye makundi.
Hivi karibuni, mtandao huo ulitangaza kuyafuta makundi yote ya watumiaji wake na watakuwa wanatumia programu ya Facebook Messenger kuchati, ikiwa ni hatua ya kuuboresha mtandao huo wa kijamii.
Maboresho hayo yanayotarajiwa kufanyika wiki hii ya Septemba 26, 2019 yatahusisha stori zote zilizokwisha wekwa na zile zitakazowekwa baada ya muda huo.
Baada ya hapo mtu aliyeko kwenye kundi husika hatokuwa na uwezo wa kuweka picha tena kwenye stori badala yake anaweza kutumia namna nyingine ya kuiweka picha hiyo kwa njia ya kawaida ndani ya kundi.
Zinazohusiana:
- Facebook yaja na tovuti ya ‘usiri’ kuwasaidia wafanyabiashara kuelewa sera zake
- Facebook yafanya maboresho utafutaji wa bidhaa mtandaoni.
Kwa mujibu wa mtandao wa Social Media Today, mabadiliko hayo yamefanyika kwa lengo la kupunguza kero za watu waliopo kwenye makundi kuweka picha zenye maudhui yasiyoendana na lengo la kundi hata baada ya waanzilishi (Admin) wa kundi kupewa mamlaka ya kudhibiti maudhui hayo.
Uwezekano wa waanzilishi wa makundi kupata tabu kudhibiti kila kinachowekwa katika sehemu hiyo umeongeza ukakasi uliowasukuma wataalam kuondoa kipengele hicho katika mtandao huo.
Hata hivyo, Facebook hawajatoa tamko rasmi la mabadiliko hayo kama yatahusisha programu yake tumishi ya Facebook Messanger.
Facebook kama ilivyo mitandao mingine ya kijamii inafanya jitihada mbalimbali za kuboresha huduma zake ili kukidhi matakwa ya watumiaji wake.
Watumiaji wengine ambao hawaweki stori kwenye makundi wataendelea kupata huduma hiyo kwenye kurasa zao kama ilivyo sasa. Picha|Mtandao.