October 7, 2024

Fanya haya kuyaokoa macho yako na athari za matumizi ya muda mrefu ya kompyuta

Kuchoka kwa macho husababishwa na matumizi ya skrini kwa muda mrefu bila kupumzika.

  • Matumizi ya kompyuta yamekuwa makubwa kadri sayansi na teknolojia inavyozidi kukua.
  • Kwa watu ambao wanafanya kazi kwa muda mrefu kwenye kompyuta, huenda wamekutana na changamoto mbalimbali iwemo kichwa kuuma.
  • Kuzuia changamoto hiyo inayosababishwa na kuchoka kwa macho, unashauriwa kupunguza muda wako katika skrini ya kompyuta yako.

Dar es Salaam. Kwa jinsi teknolojia inavyozidi kukua, matumizi ya bidhaa za kielektroniki zikiwemo simu, televisheni na kompyuta hayaepukiki.

Mathalani matumizi ya kompyuta yanatumika kama kigezo cha waajiri pale wanapotafuta wafanyakazi katika nyanja mbalimbali. Hilo limesababisha baadhi ya watu wakiwemo wasanifu kurasa na picha (graphics designers) na wahandisi programu kutumia muda mrefu katika kompyuta zao jambo linaloambatana na madhara mbalimbali ikiwemo kuchoka kwa kiungo hicho muhimu kwa kuona.

Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Mayo Clinc, kuchoka kwa macho husababishwa na matumizi ya skrini kwa muda mrefu bila kupumzika ikiwemo katika harakati za kufanya kazi na hata burudani.

Ili kuepukana na tatizo hilo ambalo husababisha kuuma kwa kichwa na kuona maruerue, inashauriwa kuyapatia macho yako wasaa wa kuangalia vitu vingine mbali na kompyuta ama kutumia miwani maalumu ya kompyuta.

Unahitaji kufahamu njia zingine rahisi? Tazama video hii kujifunza.