Gmail kuja na mabadiliko makubwa mwanzoni mwa Julai 2019
Katika maboresho hayo, kutakuwa na huduma ya kukubali au kukataa wito kwenye tukio, kujaza maswali, kujibu maoni, na orodha za kuvinjari (browsing catalogs).
- Katika maboresho hayo, kutakuwa na huduma ya kukubali au kukataa wito kwenye tukio, kujaza maswali, kujibu maoni, na orodha za kuvinjari(browsing catalogs).
- Maoni ya kwenye Google Docs sasa yatakuja moja kwa moja kwenye barua pepe ya mtumiaji ili aweze kujibu maoni hayo kwa haraka.
Dar es Salaam. Mwanzoni mwa mwezi ujao huduma ya barua pepe ya Google (gmail) itafanyiwa maboresho kwa kuongezewa kipengele kinachoitwa ‘dynamic email’ ikiwa ni moja ya mabadiliko makubwa ambayo Google imeyafanya baada ya yale ya mwaka jana ya kalenda na sehemu ya notebook (task bar) ambayo yalimfanya mtumiaji asiishie kutuma na kupokea baruapepe tu.
Mabadiliko hayo makubwa kwenye gmail, ambayo yalianza kupatikana kwa majaribio (beta version) tangu Machi mwaka huu kwa wateja wa biashara, sasa yataanza kutumika rasmi kuanzia Julai 2.
Katika maboresho hayo, mtumiaji wa barua pepe ataweza kuifanya isibadilike kwenye akaunti zake zote (default on all Gmail accounts) huku akiweza kufanya kazi kadhaa akiwa ndani ya barua pepe yake bila kuondoka na kwenda kwenye ukurasa mwingine.
Zinazohusiana:Miaka 15 ya Gmail inavyoongeza thamani bidhaa za Google
Nukta Africa yateuliwa katika mpango wa Google
Pia kwenye barua pepe kutakuwa na huduma ya kukubali ama kukataa mwaliko wa tukio maarufu kwa Kiiengereza RSVP-ing , kujaza maswali, kujibu maoni, na orodha za kuvinjari(browsing catalogs).
Itakavyofanya kazi
Badala ya kupokea ujumbe pale mtu apokutaja kwenye maoni yaliyoandikwa kwenye nyaraka za programu ya kuandika Google Docs), katika mabadiliko mapya maoni hayo yatakuja kwenye barua pepe yako ya gmail na utaweza kujibu kirahisi na kwa haraka.
Pindi huduma hiyo itakapo anza kampuni ambazo zitaweza kutumia pia ni Booking.com, Despegar, Doodle, Ecwid, Freshworks, Nexxt, OYO Rooms, Pinterest, na RedBus, huku Google ikieleza huo sio mwisho wa idadi ya watumiaji na kusisitiza huduma hiyo kwa siku za mbeleni itakuwa kwa watumiaji wote.