November 24, 2024

Google kutumia masharti mapya kwa wanaotafuta vitu mtandaoni

Itasitisha utafutaji wa taarifa zisizotumia mfumo wa (HTTPS) katika vitafutishi vilivyo chini ya kampuni hiyo.

  • Kampuni ya teknolojia ya Google imesema ifikapo Aprili 2020 itasitisha utafutaji wa taarifa zisizotumia mfumo wa (HTTPS) katika vitafutishi vilivyo chini ya kampuni hiyo.
  • Google imesema ni hatua inayosaidia kuweka usalama na usiri wa taarifa za mtu mtandaoni.

Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Google imesema kuanzia Aprili 2020 itaanza kusitisha utafutaji au upakuaji wa taarifa kutika vitafutio vya vitu mtandaoni (Browser)  visivyoendana na kampuni hiyo kwa lengo la kuhakikisha usalama na usiri wa mtu katika kutafuta mambo yake mtandaoni.

Sehemu za kutafutia vitu (Browser)  zinazomilikiwa na kampuni hiyo ni pamoja na Chrome na Mozilla Firefox ambazo hazitaruhusu kupakua taarifa zilizo nje ya utaratibu uliowekwa na Google au zisizotumia anuani ya ya mpangilio unaohakikisha usalama wa taarifa za mtumiaji (https).

Google imeeleza sababu ya maamuzi hayo kuwa ni njia rahisi ya kuweka usalama wa taarifa za wateja wake pamoja na haki ya faragha waliyonayo katika kumiliki taarifa wanazozitafuta bila kuingiliwa na mtu katikati.

Kabla ya hapo ilikuwa rahisi kwa mtu kutumia anuani yoyote kwenye vitafutishi vya Google ambapo ilikuwa inatoa mwanya kwa mtu mwingine  kuingilia kati na kupata taarifa za mtu mhusika.


Zinazohusiana:


Mtaalam wa maswala ya teknolojia Emmanuel Evance anasema hatua hiyo ni nzuri kwani uwezekano wa kuwa na waingiliaji taarifa za watu “Hackers”  utapungua kutokana na kuziba upenyo wa kupata taarifa hizo.

“Mfumo wanaouweka kwa sasa utasaidia sana kuwa na uhuru na taarifa zako kwani ni ngumu mtu kuingilia kati kujua taarifa unazozitafuta mtandaoni kwasababu taarifa zote zitakuwa chini ya mfumo wa http unaoendeshwa na Google wenyewe,”amesema Emmanuel.