October 7, 2024

Hivi ndivyo Google inavyoondoa upweke mtandaoni

Ni kupitia michezo ya mtandaoni inayoadhimisha sherehe na matukio muhimu duniani, jambo linalowafanya watu wafurahie wakati wakitumia programu za kampuni hiyo.

  • Ni kupitia michezo ya mtandaoni (Google Doodles) ambayo ilianza kurushwa Aprili 2020.
  • Doodles hizo zinatumika kuwakumbuka watu maarufu na kuadhimisha siku muhimu duniani.
  • Michezo hiyo huwafanya watu kuburudika hata wakiwa wapweke nyumbani. 

Dar es Salaam. Bila shaka kukaa nyumbani bila kitu cha kufanya ni changamoto kwa watu wengi hasa kipindi hiki cha janga la ugonjwa virusi vya Corona (COVID-19)

Hali hiyo imeifanya kampuni ya teknolojia ya Google kuibuka na kampeni ya siku kumi inayodhamiria kukupunguzia hali ya kuboreka kwa kukupatia michezo ya mtandaoni kila siku kupitia programu zake za Google Doodle.

Google Doodle ni mabadiliko ya muda mfupi yanayofanywa kwenye logo na kitafutio cha vitu mtandaoni cha Google kuadhimisha sikukuu na hata mtu fulani kwa michezo ya mtandaoni inayorandana na maadhimisho hayo.

Katika kuwafanya watu wafurahie wakati wote kampuni hiyo imezirejesha “doodle” za miaka iliyopita ili kuongeza ufanisi kwa watu wanaotumia kitafutio chake cha vitu mtandaoni. 

Kama haufahamu kampeni hiyo, hizi ndizo doodles zilizokupita tangu kampeni hiyo ianze mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2020. 

Kwa Aprili 27, ndiyo ilikuwa siku ya kwanza ya programu hiyo na ilianza kwa dhima ya  “Coding for Carrots,” ambapo doodle iliyotumika ni ile iliyoadhimisha lugha ya kwanza ya programu za kompyuta iliyotengenezwa kwa ajili ya kutumika na watoto.

Kwenye mchezo wa mtandao wa doodle hiyo, mtu aliweza kutengeneza amri kadhaa ambazo zillimuwezesha sungura kukusanya karoti kwa kila hatua (level).

Google Doodle ni mabadiliko ya muda mfupi yanayofanywa kwenye logo na kitafutio cha vitu mtandaoni cha Google kuadhimisha sikukuu na hata mtu fulani kwa michezo ya mtandaoni inayorandana na maadhimisho hayo. Picha| Giphy

Aprili 28 ilihusisha doodle ya kuadhimisha kombe la mabingwa wa mchezo wa magogo lililoandaliwa na Baraza la Kriketi la Kimataifa (International Cricket Council) ambalo linashindaniwa na wanamichezo wa mchezo wa magongo.  

Siku iliyofuata yaani Aprili 29, ilikuwa siyo mchezo wa mtandaoni bali Google waliamua kusherehekea siku ya kuzaliwa ya 117 ya  Oskar Fischinger ambaye ni mtengeneza “animation” (katuni za muziki)

Fischinger alifariki mwaka 1967 nchini marekani aliyefanikiwa kutengeneza katuni za muziki miongo mingi kabla ya kuibuka kwa video za muziki na programu za kompyuta. 

Kufunga mwezi Aprili 30, Google iliandaa mchezo mbao ungekurudisha miaka ya 1930 kwenye vyombo vya muziki vilivyopigwa kwa ueledi na Clara Rockwell ambaye chombo cha muziki kijulikanacho kama “theremin” kilikuwa ni mchezo wake.


Zinazohusiana


Doodle za mwezi Mei

Kupumzika na doodle za muziki, Google ilisherehekea Mei Mosi na Doodle yenye mchezo wa “Garden Gnomes” ambapo doodle hiyo ilitumika mwaka 2018 kwenye sikukuu ya bustani inayosherehekewa kila jumapili ya pili ya mwezi Mei.

Kwa Mei 2 na 3 ilikuwa wikiendi hivyo hakukuwa na doodle yeyote.

Jumatatu ya Mei 4, Google ilimsherehekea  Wilbur Scoville ambaye alikuwa ni mfamasia nchini Marekani kabla ya umauti kumkuta Machi 10, 1942. 

Siku iliyofuata, kampuni hiyo ya Marekani katika kitafutio chake cha  Google iliadhimisha vilivyo tamaduni za watu wa Mexico kupitia doodle ya Lotería ambao ni mchezo kama ulivyo mchezo wa Bingo ambao wenyewe unatumia kadi badala ya namba.

Mei 6 Google ilikumbushia sikukuu za Haloween ya mwaka 2016 ambazo zinasherehekewa kwa kuvalia nguo za kutisha kwa “Magic Cat Academy” huku jana iliamua kuwapa heshima wanamuziki wa kufoka maarufu kama Hip Hop. 

Leo, Google imeandaa doodle yenye mchezo wa PackMan ambayo ilitamba mwaka 2010.

Kama doodle za zamani zimekupita, tembelea ukurasa wa Google doodle kupata nafasi ya kucheza na doodle zilizopita.