October 7, 2024

Huduma za Google zapata hitilafu

Mpaka sasa haijulikani sababu ya huduma hizo kutopatikana.

  • Baadhi ya watumiaji wake wanalalamika kutopata huduma hizo mtandaoni.
  • Mpaka sasa haijulikani ni sababu gani ambazo zimesababisha hali hiyo. 

Dar es Salaam. Baadhi ya huduma za kampuni ya teknolojia ya Google ikiwemo baruapepe ya Gmail hazipatikani mtandaoni, jambo ambalo limeibua usumbufu kwa watumiaji wa huduma hizo.

Huduma nyinginge ambazo baadhi ya watu wanalalamika kutozipata kuanzia mchana wa leo Desemba 14, 2020 ni mtandao wa YouTube, sehemu ya kuhifadhia nyaraka mtandaoni ya Google Drive na Google doc inayotumika kuandikia nyaraka mbalimbali.

Kwa kila anayetaka kufungua huduma hizo anakutana na ujumbe unaosema ” Samahani, akaunti yako haipatikani. Samahani kwa usumbufu uliotokea na jaribu tena baadaye.”

Mpaka sasa haijulikani ni changamoto gani imetokea kwa huduma hizo kutopatikana.

Pia watumiaji katika mataifa mengine wamelalamika kwa kukosa huduma hizo.


Soma zaidi:


Google imewaelekeza watumiaji wa huduma zake kutembelea kituo cha msaada cha kampuni hiyo yenye makao makuu nchini Marekani kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.

Mtandao wa YouTube ni moja ya huduma maarufu ya Google inayowapatia fursa watumiaji wa mtandao kutazama na kusikiliza muziki na kupata habari za televisheni mtandao.

Pia, Google imekua ni kiungo muhimu kwa watu wanaofanyia kazi au biashara mtandaoni kwa sababu ni njia ya rahisi ya kuwasiliana na kutunza nyaraka.