October 7, 2024

Instagram kumuwezesha mtumiaji kupata kumbukumbu za video kwa urahisi

Mtandao huo umekuja na maboresho mapya yanayomwezesha mtumiaji kupata kumbukumbu za matukio ya video yaliyopita.

Maboresho yatakayofanyika hivi karibuni na mtandao wa instagram. Picha| Google.


  • ​​​​​​​Mtandao huo umekuja na maboresho mapya yanayomwezesha mtumiaji kupata kumbukumbu za matukio ya video yaliyopita.
  • Maboresho hayo yatasaidia kuunganisha matukio mbalimbali ya zamani na mapya ili kuleta mpangilio mzuri wa kumbukumbu.

Dar es Salaam. Instagram ni moja ya mitandao ya kijamii maarufu duniani unaotumika na watu mbalimbali  kuwasiliana na kuunganisha watu. Sifa kuu ya mtandao huo ni kuwawezesha watumiaji kuweka picha pamoja na video na zikaonekana kirahisi na watu. 

Ili kuendana na ushindani uliopo na mitandao mingine yenye sifa kama zake ikiwemo Facebook, Twitter na hata snapchat, matando huu unazidi kuleta mabadiliko kila baada ya muda mfupi kwaajili ya kuwavutia watumiaji wengi zaidi.

Safari hii mtandao huo umekuja na maboresho mapya yanayomwezesha mtumiaji kupata kumbukumbu za matukio ya video yaliyowahi kuwekwa katika mtandao huo na mtu yeyote kwa urahisi.

Maboresho hayo yatasaidia kuunganisha matukio mbalimbali ya zamani na mapya ili kuleta mpangilio mzuri wa matukio ikizingatiwa mtumiaji anaruhusiwa kuweka video isiyozidi urefu wa dakika moja.  

Kwa sasa, baada ya kuweka video ama picha hiyo ya muda mfupi, mtumiaji anaweza kuirejea tena hata baada ya muda wake kupita hivyo kuleta mfumo wa albamu ya matukio mbalimbali ya mtumiaji

Pamoja na maboresho hayo, mtandao huo umeweka udhibiti wa kutosha wa maudhui ya video na picha  utaokaosaidia kuepusha matumizi mabaya ya mtandao huo unaotegemewa na watu wengi kufikisha ujumbe au taarifa kwa watu wao wa karibu. 

Instagram haijatoa tamko rasmi ya lini maboresho haya yatafanyika lakini yatakua maboresho yatakayosaidia watumiaji wake hasa katika suala zima la kutunza kumbukumbu za mtuamaji.