Instagram yafungua fursa kwa wazalishaji maudhui mtandaoni
Mtandao huo umetangaza hatua mpya ya kuifanya televisheni yake ya IGTV kuwa kibiashara zaidi (next stage of monetization for IGTV) ili watumiaji wapate fedha kupitia matangazo.
- Mtandao huo umetangaza hatua mpya ya kuifanya televisheni yake ya IGTV kuwa kibiashara zaidi (next stage of monetization for IGTV) ili watumiaji wapate fedha kupitia matangazo.
- Itagawana mapato ya matangazo na wazalishaji maudhui yatakayopatikana.
Mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika zaidi kwa watu kuwasiliana na kuimarisha mahusiano kwenye jamii, lakini ni wachache ambao wameenda mbali na kuitumia kibiashara.
Kama bado unafiriki unakwama wapi kutengeneza kipato kupitia mitandao ya kijamii basi Instagram ina mpango kwa ajili yako.
Mtandao huo umetangaza hatua mpya ya kuifanya televisheni yake ya IGTV kuwa kibiashara zaidi (next stage of monetization for IGTV) ili watumiaji wapate fedha kupitia matangazo.
Television hiyo ya kidijitali hutoa fursa kwa watumiaji kurusha vipindi vyao mubashara na kuvirekodi kwa matumizi ya baadaye.
Kwa sasa inaongeza beji ya kidijitali kwenye IGTV ambayo itawawezesha watazamaji kuchangia pesa kwa watangazaji wanaowapenda.
Ilianza kufanya majaribio tangu February mwaka huu ambapo Machi iliwakaribisha baadhi ya watengeneza maudhui ili kufahamu kama watapata matokeo halisi.
Na sasa wametangaza rasmi kuifanya televisheni hiyo kuwa kibiashara.
Unapate pesa kupitia IGTV?
Katika taarifa take iliyotolewa mwishoni mwa wiki, Instagram imesema itakuwa inaweka matangazo kwenye maudhui ya watumiaji wa IGTV ili kutangaza biashara za watu na kampuni mbalimbali.
“Matangazo ya IGTV yatakuwa yanaonekana ikiwa mtu anataka kutazama video ya hadi sekunde 15 lakini tutapitia kwa umakini ili kuhakikisha mtu anakuwa na uhuru wa kutokuandalia tangazo husika,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Instagram itagawana mapato ya matangazo na wazalishajimaudhui, jambo litakalowavutia kuzalisha maudhui mengi na kuongeza ushindani kwa watumiaji wa mtandao huo.
Kwa kuanzia wazalishaji maudhui watapata asilimia 50 ya mapato ya matangazo ya IGTV kama ilivyo kwa YouTube.
Zinazohusiana:
- Instagram yazindua akaunti maalumu ya kuuza bidhaa mtandaoni
- Facebook, Instagram ‘kufichua’ kiwango cha muda unaotumika mtandaoni
Hii ni fursa kwa watumiaji wa Instagram kuwashawishi wafanyabiashara na kampuni kuweka matangazo kwenye televisheni hiyo ile wapate kipato.
Irene Joseph, mkazi wa Morogoro ambaye ni mtumiaji wa Instagram ameiambia Nukta (wwww.nukta.co.tz) kuwa ni hatua nzuri ya kuifanya Instagram kuwa jukwaa linalowaidisha watumiaji wake.
“Ni jambo jema hilo maana watu wanatumia mwingi kuzalisha maudhui lakini wanaishia kupata likes na maoni mengi. Lakini sasa angalau watapata pesa,”