July 8, 2024

Jinsi ya kufuatilia utendaji wa akaunti zako za mitandao ya kijamii

Teknolojia inakupa zana (Tools) rahisi za mtandaoni zinaweza kukupa taarifa muhimu za matumizi.

  • Teknolojia inakupa zana (Tools) rahisi za mtandaoni zinaweza kukupa taarifa muhimu za matumizi ya mitandao ikiwemo idadi ya wafuasi, maeneo wanakopatikana na mambo wanayopenda. 
  • Pia zana hizo zinakuwezesha kulinganisha biashara yako na washindani wako.

Dar es SalaamMatumizi ya mitandao ya kijamii hayaepukiki tena katika zama hizi ambazo duniani inashuhudia mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia. 

Mitandao ya kijamii siyo tu inatumika kuwasaliana lakini wafanyabiashara na kampuni hutumia kwa ajili ya kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa. 

Lakini unafahamu zana za msingi (Analytics tool) zinaweza kukusaidia katika mipango na utendaji wa mitandao ya kijamii? Dhana hizo za kuwezesha ni nyenzo muhimu katika kufahamu ni maeneo gani yanafanya vizuri katika kuwafikia watu na ni maeneo gani unahitaji kuongeza nguvu ili kuhakikisha mitandao ya kijamii inafanikisha shughuli zako. 

Nukta (www.nukta.co.tz) inakuletea zana zitakazokusaidia kupima mwenendo wa utendaji wa mtandao unaotumia kuwafikia watu kwa kutumia takwimu. 

Awario

Zana hii inafuatilia kwa kaisi gani jina lako la biashara limetajwa katika mtandaoni ili kuweza kukuasaidia kupata takwimu sahihi za biashara yako ilipotajwa, imewafikia watu wangapi, imetajwa katika lugha ngapi na katika tovuti gani .

Pia inasaidia kujua katika mitandao ya kijami nani anayetumia neno lako la kibiashara au bidhaa. Vilevile inakuonyesha orodha ya walagabishi waliotumia maneno yako.

Zana hiyo pia inaweza kuset alamu kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa jina lako la kibiashara dhidi ya washindani wako mtandaoni kwa kutumia chati kwa kuonyesha kiasi kinachozalishwa kwa katika biashara.

Muonekano wa mtandao wa  Awario unotumika katika kufuatilia mwenendo wa mitandao ya kijamii. Picha|Mtandao.

Snaplytics

Zana hii  ya pili kazi yake ni kutoa data ya utendaji wa kina kwa mitandao ya kijamii ya Instagram na Snapchat ambapo humuwezesha mtumiaji kufahamu ukuaji wa habari zake sambamba na ukuaji wa wafuasi wake

Kwa kutumia Snaplytics unaweza kuona kwa urahisi nini kilicho sababisha habari yako kuvuma kwa haraka  au kufifia  kwa haraka kwa kujua huko kutakusaida kujua utumie mbinu gani.

Kupitia zana hiyo mtuamiaji ana weza kupata ripoti za takwimu kutoka katika mtandao wake wakijamii ikiwa katika faili la CSV.


Soma zaidi:


Squarelovin

Squarelovin imetengenezwa mahususi kwa ajili ya Instagram. Kinasaidia kutambua mtu au taasisi ina  wafuasi wangapi na kuafuatilia mwenendo wa habari na ushiriki wa watu katika ukurasa wa  instagram yako  (reviews post performance and measures). 

Pia inaonyesha nyakati bora za kuchapisha, ‘filters’ na Hashtag bora za kutumia pamoja na historia ya machapisho yako yakiwa kwa mtindo wa saa. Unaweza pia kupata ufahamu zaidi wanaokufuatilia katika mtandao Instagram na vitu wanavyopendelea.

Squarelovin imekuwa ni zana muhimu kuwafikia watu wengi mtandaoni. Picha|Mtandao.

Rival IQ

IQ inafanya uchambuzi wa machapisho, vipendwa (likes) na maoni kutoka kwenye mitandao mikubwa ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, na Pinterest. Rival IQ ikiunganishwa na ‘Google Analytics’ inaweza kuonyesha picha kamili ya jinsi wateja wako wanavyokufikia, na wanachofanya nini pale  wanapofika.

Pia inachambua matangazo ya Facebook na Instagram ili kuhakikisha kwamba watangazaji  unanufaika zaidi pia inasaidia kujua washindani wako  wana nguvu sehemu gani ili uweze kuwashinda. 


Wiselytics

Inashughulikia zaidi zamitandao ya Facebook na Twitter. Inaonyesha takwimu za muhimu (metrics)  kwa majukwaa haya mawili  ikiwemo jinsi ya kuwafikia watu na ushiriki wao. Inatoa fursa sawa kwa washindani, na inasaidia kujua mada inayozungumzwa zaidi katika mitandao hiyo.


Inawezesha kutambua mada ambayo imewafikia zaidi na wafuasi wako. Wiselytics huzalisha ripoti za ‘PowerPoint’ kwa kubonyeza mara moja tu katika lugha moja ya sita.