July 8, 2024

LinkedIn yaja na fursa ya matangazo kwa wafanyabiashara wadogo

Sasa wafanyabiashara wadogo wataweza kuorodhesha huduma wanazotoa kwenye wasifu wao wa LinkedIn.

  • Wafanyabishara wadogo kuorodhesha huduma wanazotoa kwenye wasifu wao wa LinkedIn ili kuvuna wateja.

Mtandao wa  kijamii wa LinkedIn wenye watumiaji wapatao milioni 600 ulimwenguni umeanzisha kipengele kipya kitakachowawezesha watumiaji binafsi (freelence) pamoja na wafanyabiashara wadogo kuorodhesha huduma wanazotoa kwenye wasifu wao wa LinkedIn, kisha bidhaa hizo kuonekana pale mtu anapowatafuta.

Kipengele hicho kitawawezesha watumiaji wa mtandao huo kuweza kuongeza taarifa nyingine kwenye kurasa zao ambapo wataweza kuonyesha huduma zao wanazozitoa.

Pia, LinkedIn imefanya mabadiliko kwenye huduma ya utafutaji wake (Search option) ambapo mtumiaji wa mtandao huo anaweza pia kuwapata wafanyabishara wanaotoa huduma moja pale atakapotafuta kwenye LinkedIn. 

Kwa sasa mabadiliko hayo  hayajaanza kupatikana kwa watu wote ulimwenguni lakini mtumiaji wa mtandao huo anaweza kuongeza kipengele hicho mwenyewe katika wasifu wake kwa kutumia simu au kwenye kompyuta.

Mtumiaji huyo ataona kisanduku chini ya picha ya wasifu wake kitakacho  mwonyesha ni kwa namna gani ataweza kuonyesha huduma unazozitoa.

Mwonekano wa kipengele kipya  kitakachowawezesha watumiaji binafsi (freelence) pamoja na wafanyabiashara wadogo kuorodhesha huduma wanazotoa kwenye wasifu wao wa LinkedIn.Picha|LinkedIn.


Zinahusiana: Twitter kuwawekea watumiaji wake muonekano mpya


LinkedIn imewashauri  watumiaji wa mtandao huo wajaze kwa umakini na kwa upana ilikuwezesha huduma zao  kujulikana ipasavyo. Mtumiaji akisha jaza fomu hizo atatakiwa kubonyeza kuedelea na atakuwa umeshaingia moja kwa moja.

Hata hivyo, LinkedIn haijaeleza iwapo matangazo hayo yanatakiwa kulipiwa ama la kwa sasa.

Tangu mtandao huo uanzishwe mwaka 2003 umeendelea kufanya mabadiliko mbalimbali ili kukidhi matakwa ya watumiaji wake katika kipindi hichi ambacho teknolojia imekuwa ikikua kwa  kasi sana ulimwenguni kote. 

Mwonekano wa kipengele kipya  kitakachowawezesha watumiaji binafsi (freelence) pamoja na wafanyabiashara wadogo kuorodhesha huduma wanazotoa kwenye wasifu wao wa LinkedIn.Picha|LinkedIn