November 24, 2024

Programu zitakazokusaidia kutunza kumbukumbu mtandaoni

Kupitia teknolojia hizo, mtu anaweza kuhifadhi nyaraka muhimu, video na miziki aipendayo bila kuhofia kupotea.

  • Mifumo hiyo ni kama Google drive na dropbox ambayo inaweza kuhifadhi kumbukumbu zako mtandaoni.
  • Inasaidia hasa pale endapo kifaa chako kama simu au kompyuta kikipotea au kuharibika.
  • Usalama wake dhidi ya wadukuzi ni suala la kuzingatia endapo unahifadhi taarifa nyeti.

Dar es Salaam. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamerahisisha uwezo wa watu kuhifadhi kumbukumbu zao kwa kutumia vifaa mbalimbali vikiwemo kompyuta, flashi na hata simu za mkononi.

Kupitia teknolojia hizo, mtu anaweza kuhifadhi kuanzia nyaraka muhimu, video na miziki aipendayo. Lakini vifaa hivyo vikiharibika, kupotea au kuibiwa, kumbukumbu zote hupotea.

Hali hiyo imekuwa ikiwasononesha watu waliokumbwa na matukio hayo. Lakini wabunifu wamekuletea mifumo ya utunzaji vitu vyako mtandaoni ambako usalama ni mkubwa na wa uhakika. 

Hata kifaa chako kikiharibika, unaweza kuzipata nyaraka zako kwa kifaa kingine zikiwa salama. Baadhi ya teknolojia hizo ni pamoja na:

Google Drive

Google Drive ni moja ya bidhaa za Google ambayo inapatikana kwa watumiaji wa barua pepe zenye mfumo wa G mail. Kupitia mfumo huu,mtu anaweza kuhifadhi picha, hati na hata viedeo.

Kwa kuanzia, mtumiaji wa mfumo huu atapewa nafasi yenye Jigabaiti (GB) 15 za bure na endapo atazimaliza, atahitajika kufuta vitu au kufanya manunuzi ya nafasi ya ziada.

Kwanza unatengeneza kablasha “folder” na kisha ukiingia kwenye kablasha lako, unaweza kuongeza kumbukumbu zako na kuzihifadhi. 

Hata baada ya nafasi yako ya megabaiti 15 (GB15) kuisha, bado una uwezo wa kuongeza nafasi kwa kukunua  nafasi inayogharimu Sh4500 kwa mwezi na Sh45,000 kwa mwaka kwa GB 100.

Ili utumie Google Drive unatakiwa uwe na barua pepe ya Gmail ambayo nayo iko chini ya Google.

Wakati Dropbox ikitoa GB mbili pekee kwamtu anayetumia akaunti ya bure, Google drive inatoa GB15. Picha| Dreamstime

PCloud

Mbali na kuwa na GB 10 za bure kwa mtumiaji anayeanza,programu hii ya uhifadhi unakupatia uwezo wa kutazama vitu ulivyohifadhi endapo umeunganishwa na mtandao bila uhitaji wa kuvipakua.

PCloud ambayo inafanya kazi kama mifumo mingine, ina changamoto moja ambayo baadhi ya watumiaji wameisema mtandaoni. Changamoto hiyo ni kuwa kuna vitu vingine havipatikani kwenye mfumo wa bure, hadi ulipie.

Mfumo huu wa uhifadhi unaanzia GB 10 ya bure chini ya ile inayotolewa na Google. PCloud ina uwezo wa GB 500 inayogharimu Sh9,213 na kisha TB mbili ambazo zinagharimu Sh18,449 kwa mwezi.


Zinazohusiana


Programu tumishi ya Dropbox

Programu tumishi ya simu (App) hii inakupatia GB mbili tu za bure na unaweza kuongeza uhifadhi hadi kufikia Terabaiti tano  (TB5).

Kuhifadhi kumbukumbu zako kwenye teknolojia hii unahitaji kuipakua kwenye duka lako la programu na kisha kusajili akaunti yako. Baada ya hapo, kama ilivyo kwenye Google Drive, unaweza kutengeneza kablasha na kisha kuanza kufurahia nafasi yako ya GB 2.

Endapo nafasi hiyo ikiisha, unaweza kununua kwa Sh46,158 kwa nafasi ya TB mbili. 

Kwa mfumo huu wa uhifadhi, kumbukumbu zako zinakuwa salama kila, hata ikibadilisha au kununua kifaa kipya bado utazikuta mtandaoni.


Mfumo wa  I Drive

Teknolojia hii inaanza na uwezo wa GB tano za bure lakini endapo utaona hizo hazikutoshi, unaweza kununua GB 250 kwa Sh344,633 kwa miaka miwili au kama utahitaji zaidi, ni vyema mfuko wako ukawa na uzito wa Sh1.7 milioni kwa nafasi yenye ukubwa wa TB 1.25.

IDrive inaweza kutumika na watumiaji wa vifaa vinavyotumia mifumo endeshi ya Android, na hata wenye kompyuta na simu za kampuni ya Apple. Kwa sasa, huduma hii ipo kwenye promosheni.

Wadau wateknolojia wamesema ni bora kuwa makini kwani mifumo hii ya uhifadhi ni rahisi kudukuliwa. Picha| Channelfutures

Degoo Cloud

Wadau mbalimbali ikiwemo tovuti ya techradar wanasema huu ni mfumo unaosadikika kuwa na nafasi kubwa zaidi kwenye huduma ya bure ya kuanzia.

Degoo ambayo ni ngeni kati ya mifumo ya kuhifadhi kumbumbuku inampatia mtumiaji nafasi ya GB100 za bure na kisha kumlazimu mtu kulipia pale ambapo hazitamtosha.

Licha ya kwamba safari ya kulipia ni ghali ikilinganishwa na mifumo mingine, Degoo imesemekana kuwa kati ya mifumo salama kwa uhifadhi wa kumbukumbu.

zaidi, wadau wanashauri kuwa makini pale unapoweka taarifa zako mtandaoni.

wadau wa teknolojia wanashauri kuwa, mbali na uhalisia wa kwamba unakua kama mpangaji kwa kulipa kodi ya mwezi au mwaka, mifumo hii inategemea intaneti

Kirahisi ni kusema, bila intaneti, hauwezi kupata taarifa zako pale utakapozihitaji. Pia amezungumzia changamoto ya kiusalama.

Inashauriwa, endapo hakuna mifumo maalumu ya kuziweka nyaraka zako faragha (Encryption) basi kunakuwa hakuna usiri wa taarifa zako. Wahandisi wa mifumo hiyo wanakuwa na uwezo wakuziona taarifa zako..

Hata hivyo, ni rahisi kwa wadukuzi kudukua akaunti zako za mtandaoni endapo wakidhamiria, kwa taarifa ambazo ni nyeti hasa kwa makampuni na hata binafsi, unashauriwa kutafuta njia salama zaidi.