October 6, 2024

RC Makonda azindua mfumo wa kutoa malalamiko Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amezindua mfumo wa kidijitali wa kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu au kompyuta ili ujumbe uwafikie watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda m

  • Mfumo huo wa kidijitali  utawawezesha wananchi wa mkoa huo kuwasilisha kero zao kirahisi kwa viongozi.
  • Unalenga kutatua changamoto ya kutokuwa na mahali pa kupeleka malalamiko yako kama mtu binafsi pindi unapopatwa na tatizo.
  • Itasaidia kuokoa muda na gharama za kuwafikia viongozi wa mkoa huo.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amezindua mfumo wa kidijitali wa kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu au kompyuta ili ujumbe uwafikie watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi. 

Makonda aliyekuwa akizindua mfumo huo leo (Oktoba 10, 2019) Jijini Dar es Salaam amesema mkoa umefikia hatua hiyo baada ya kuona wananchi wengi wanapata wakati mgumu katika kutoa malalamiko na changamoto wanazokutana nazo ndani ya mkoa.

Lakini pia, viongozi wamekuwa hapatikani kirahisi kutatua kero mbalimbali zinazotolewa na wanachi. 

“Badala ya kuwa tu DSM (Dar es Salaam) tumeamua kukufikia kirahisi, kwa lugha nyepesi ni kuwa mkoa umeamua kuhamia nyumbani kwako,” amesema Makonda.

Mfumo huo utatumia ujumbe mfupi wa maneno wa simu za kawaida ambapo mtu yeyote anaweza kutuma ujumbe huo ili uwafikie viongozi wa mkoa, popote alipo bila kuhitaji kwenda ofisini. 

Mfumo huo umelenga kutatua changamoto ya kutokuwa na mahali pa kupeleka malalamiko yako kama mtu binafsi pindi unapopatwa na tatizo linalotakiwa kufikia uongozi kwa muda fulani.

Pia unaokoa gharama na muda ambao mtu angetumia kuwatafuta viongozi au anapohitaji msaada kwa jambo la dharura katika eneo lake.


Soma zaidi: 


Hatua hiyo ya Makonda ni mwendelezo wa mikakati yake ya kuwawezesha wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kupata huduma za kijamii kwa haraka na urahisi zaidi ili kuwawezesha kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya uzalishaji mali na kukuza kipato.

Agosti, 2019, Makonda alinukuliwa akisema kuna mpango wa kuanzisha kanzi data ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.

Kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanawake kuumizwa hivyo wakati umefika wa kuanza kushughulikia.