October 7, 2024

TBS mwendo mdundo utoaji huduma kidijitali

Yazindua mfumo wa kielektroniki wa kusajili bidhaa, majengo na maeneo ya uzalishaji.

  • Yazindua mfumo wa kielektroniki wa kusajili bidhaa, majengo na maeneo ya uzalishaji. 
  • Utasaidia kuokoa muda na gharama kwa waombaji na kupunguza usumbufu wa usajili uliokuwa unajitokeza hapo awali.

Dar es Salaam. Shirika la viwango Tanzania (TBS) katika kuboresha huduma zake, limekuja na mfumo mpya kielektroniki unaowaweza wananchi kupata huduma ikiwemo kufanya usajili wa bidhaa, majengo na maeneo ya uzalishaji mtandaoni.

Mfumo huo unaojulikana kama ‘TBS Online Application System (OAS)’ huenda ukawapunguzia usumbufu waombaji waliokuwa wanatumia mfumo wa kawaida na kuwawezesha kuokoa muda na gharama za usafiri kwenda kufuata huduma hiyo TBS. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TBS, mfumo huo ulianza kutumika rasmi Septemba 1, 2019 ambapo kwa sasa wateja wote wanaotaka huduma za usajili watatumia mfumo huo wakiwa popote nchini.  


Zinazohusiana:


Ili mtu aanze kutumia mfumo huo anapaswa kujisajili na kuwa na akaunti katika mfumo wa ‘OAS’ uliopo katika tovuti ya TBS na kufuata taratibu zote zilizowekwa ili kufanikisha maombi yake. 

Mabadiliko ya teknolojia, yamerahisisha maisha. Taasisi za umma na binafsi zinachukua hatua mbalimbali kutumia mifumo ya kidijitali ili kurahisisha utoaji wa huduma na bidhaa na wakati huo huo kuongeza mapato ya kampuni.