July 8, 2024

Twitter yaja na mpango wa kuwaamsha watumiaji wenye akaunti zilizolala

Baada ya Twitter kubaini uwepo wa akaunti nyingi ambazo hazitumiki (Inactive accounts) katika mtandao wake, imekuja na mpango mkakati utakaowaamsha watumiaji wenye malengo wa kuendelea kuwa na akaunti hizo.

  • Utaanza Desemba 11, 2019
  • Utahusisha watumiaji wasiotumia akaunti zao pamoja na wale waliofariki.

Dar es Salaam. Baada ya Twitter kubaini uwepo wa akaunti nyingi ambazo hazitumiki (Inactive accounts) katika mtandao wake, imekuja na mpango mkakati utakaowaamsha watumiaji wenye malengo wa kuendelea kuwa na akaunti hizo.

Zoezi hilo litaanza kufanyika kuanzia kwanzia Desemba 11, 2019 ikiwa ni muendelezo wa mabadiliko mbalimbali inayofanya ili kuboresha mtandao huo na kuhakikisha watumiaji wanaenenda na sheria na taratibu za mtandao huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao wa The Verge Novemba 26, 2019 imesema utaratibu huo utawahusu wale wote wasiotumia akaunti zao kwa muda mrefu na wale waliofariki dunia.

“Kama moja ya jukumu la kuwatumikia watumiaji wetu, tunapanga kufuta akaunti zote zisizotumika kwa muda mrefu. Mkakati huo umeletwa kwa lengo kubwa la kuwatia moyo watumiaji wote kutumia vizuri mtandao huo”, imesema taarifa hiyo.


Zinazohusiana


Mkakati huo utakuwa wa muda mrefu ili kuhahakisha zoezi la kuuhisha akaunti unakuwa wa mafanikio kwa kuzingatia haki za watumiaji wake. 

Lakini kwa akaunti ambazo hazitafanikiwa kuuhishwa labda kwa sababu watumiaji wake wamefariki zitafutwa na kuondolewa kabisa.

Mkakati huo umeenda sambamba na mabadiliko katika usajili kwenye mtandao huo kutumia herufi zaidi ya tano katika jina linalofungua akaunti hiyo kwenye mtandao huo wa Twitter.