November 24, 2024

Twitter yazindua tena programu mpya ya Mac

Twitter imetangaza kuanza kutumika tena kwa programu endeshi ya Twitter (Twitter app) kwa ajili ya simu na kompyuta za Mac ambayo inapatikana katika duka la mtandaoni la Apple la App store.

  • Ni baada ya kuifunga tangu mwaka jana.
  • Imesema programu hiyo itawasaidia watumiaji wa kompyuta na simu za Mac kuvinjari mtandaoni. 

Watumiaji wa kompyuta na simu za Mac zinazotengenezwa na kampuni ya Apple, sasa wana kila sababu ya kutabasamu kwa sababu Twitter imewakumbuka tena. 

Twitter imetangaza kuanza kutumika tena kwa programu endeshi ya Twitter (Twitter app) kwa ajili ya simu na kompyuta za Mac ambayo inapatikana katika duka la mtandaoni la Apple la App store. 

Juni mwaka huu, Twitter ilitangaza kuirejesha tena programu hiyo ikiwa  imeboreshwa zaidi ili iendane na mfumo endeshi wa macOS Catalina unaotumiwa na Mac. 

Hatua hiyo ya kuirejesha tena programu hiyo inatokana na malalamiko ya watu waliokuwa wanaitumia baada ya kuifunga Februari, 2018. 


Zinazohusiana:


Kwa sasa watumiaji watafaidika na vipengele vya ziada vilivyongezwa ikiwemo kuangalia jumbe na picha kwa wakati mmoja na kutengeneza twitt nyingi kadiri itakavyo kwenye Windows tofauti.  

Pia unaweza kuwekwa moja kwa moja picha, maandishi na viunganishi sehemu ya kuandikia bila usumbufu wowote. 

Katika taarifa yake Twitter, imeeleza kuwa itaendelea kuboresha mtandao wake ili kukidhi mahitaji na matamanio ya wafuasi wake ambao wako katika maeneo mbalimbali duniani.