October 7, 2024

Unatoa harufu miguuni? Tumia viatu hivi

Ni viatu aina ya skechers vilivytengenezwa kwa teknolojia inayoondoa jasho linalosababisha harufu kwenye miguu.

  • Ni viatu aina ya skechers vilivytengenezwa kwa teknolojia inayoondoa jasho linalosababisha harufu kwenye miguu.
  • Pia vinawafaa watu wanaofanya mazoezi, kusimama muda mrefu. 
  • Watalaam wa afya waeleza jinsi ya kuvitumia ili vilete matokeo yaliyokusudia. 

Dar es Salaam. Nilipokuwa mdogo, aliwahi kuja mgeni nyumbani licha ya kuwa nilifurahia ujio wake, furaha yangu ilitetereka baada ya mgeni huyo kuvua viatu vyake. 

Harufu isiyovumilika ilitawala chumba ambacho nilikuwa nikilala na kufanya usiku wangu kuwa mrefu sana.

Hivi karibuni nikiwa katika matembezi yangu madukani, nilikutana na matangazo juu ya viatu ambavyo havitoi harufu mbaya, jambo lililonikumbusha tukio hilo lililonikuta zaidi ya miaka 10 iliyopita. 

“Nilichekwa na kutengwa sana na familia yangu ukizingatia mimi ni mwanamke, miguu yangu ilikua inatoa jasho mno na harufu ilikua kali sana. Kila aina ya mbinu nilitumia, dawa, kuomba ushauri na hata kubadili aina za viatu lakini haikusaidia,” anaeleza Nanael,  mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye anasumbuliwa na tatizo la miguu kutoa harufu mbaya. 

Nanael ambaye hakupenda jina lake la pili liwekwe wazi amesema sasa amepata suluhisho baada ya kupata viatu vyenye uwezo wa kukata harufu iliyokuwa ikitoka kwenye miguu.

“Ukinunua kiatu hicho una uhakika wa kukaa nacho miaka minne hadi mitano. Changu tangu nimenunua sijafua kwa sababu hakichafuki,” amesema Ally. Picha| Ntuli Amani.

Viatu hivyo vinafanyaje kazi?

Viatu hivyo vinavyojulikana kama “skechers shoes” vinapatikana katika maduka ya Skachers Tanzania, vimetengenezwa kwa teknolojia inayofahamika kama “memory foam” ambayo wakati wa kipindi cha joto viinatoa baridi ambayo inazuia miguu kutokutoa jasho na harufu mbaya. 

“Vinabadilika kutokana na hali ya joto ya mguu wako, ukivivaa hakuna jasho litakalokusumbua,” amesema balozi wa viatu hivyo Tanzania, Meena Ally.

Ili kupata viatu hivyo, utalazimika kutoboa mfuko wako na kutoa fedha isiyopungua Sh100,000 ili kuvaa viatu hivyo ambavyo vina kitambaa maalumu kinachopitisha hewa na uwezo wa kustahimili uzito wowote alionao mvaaji.

“Ukinunua kiatu hicho una uhakika wa kukaa nacho miaka minne hadi mitano. Changu tangu nimenunua sijafua kwa sababu hakichafuki,” amesema Ally.

Wataalam wazungumzia tatizo la harufu ya miguuni

Tovuti ya huduma za afya wa Web MD inaeleza kuwa miguu kutoa harufu ni matokeo ya kutokwa na jasho na kisha jasho hilo kukutana na soksi ama viatu.

“Sababu zipo mbili moja ikiwa ni miguu kutokwa na jasho jingi na viatu kuwa na unyevu nyevu. Pale jasho linapokutana na bakteria waliopo kwenye viatu vyako, inatengeneza harufu,” inasomeka sehemu ya tovuti hiyo.


Soma Zaidi


Mtaalam wa afya kutoka kituo cha afya cha TMH kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Dk Isaac Maro amesema kiatu hicho kinaweza kuwa msaada kwa watu wenye matatizo mbalimballi ya kiafya yakiwemo ya kiharusi, matatizo ya fangasi na hata wenye uzito mkubwa na matatizo ya mgongo.

Dk Maro ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa teknolojia iliyotumika kutengeneza kiatu hicho imeenda mbali zaidi kwa kujali afya ya mtumiaji wake. 

“Kwa watu wenye kiharusi, kipindi wanafanya mazoezi kiatu cha Skechers kitawafaa kwa sababu ni chepesi na hauwezi kuuhisi uzito wake,” amesema Dk Maro.

Amesema pia kinawafaa watu watu wanaofanya mazoezi na wanaotembea umbali mrefu na hata wale wanaosimama muda mrefu.

Habari hii imeandikwa na Rodgers George na mwanafunzi wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (TUDARCo), Leila Siraj .