July 8, 2024

Window 95 yaja kivingine baada kutoweka sokoni kwa miaka 18

Sasa watumiaji wa kompyuta wanaweza kuipakua na kuitumia kama programu tumishi (App) kucheza michezo (games).

Sehemu ya programu tumishi ya Window 95. Picha|Verge


  • Sasa watumiaji wa kompyuta wanaweza kuipakua na kuitumia kama programu tumishi (App) kucheza michezo (games).
  • Sasa ipo kama programu tumishi (Application) na inapatikana kwenye Windows 10, Linux au MacO.

Baada ya kutoweka sokoni kwa miaka 18, mfumo wa uendeshaji kompyuta la ‘Window 95’ lilotengenezwa na kampuni ya teknolojia ya  Microsoft ya nchini Marekani, sasa umerudi kwa mtindo mwingine. 

Toleo hilo la Window 95 lililoingia sokoni Agosti 15, 1995 lilibadilisha kabisa mfumo wa programu ya uendeshaji wa kompyuta na kufanya utumiaji kifaa hicho kwa wakati huo kuwa mrahisi zaidi, ikiwemo kutumia mtandao wa intaneti, kucheza michezo ya kompyuta (Game) na uanzishwaji wa ‘briefcase’ kabla ya kuja dropbox.

Lakini lilidumu sokoni kwa miaka sita tu na ilipofika 2001 liliondolewa na matoleo mengine yenye muonekano na uwezo mkubwa yakaletwa ili kurahisisha matumizi ya kompyuta. 

Sasa ikiwa imepita miaka 24 tangu kutolewa kwa mfumo huo, Window 95 imerudi kwa namna nyingine kama programu tumishi (Application) ambayo mtumiaji wa kompyuta ataweza kuipakua kwenye kompyuta inayotumia Windows 10, Linux au MacOS na kisha kuitumia kwa urahisi tuu.


Zinazohusiana: Mambo muhimu yatakayozisaidia kampuni zinazochipukia Tanzania kukua

                           Startups za Tanzania zilizotamba mwaka 2018


Mtumiaji akifanikiwa kupakua faili hilo litakuwa na  ukubwa wa 129Mb (Megabites) ambapo viunganishi wezeshi kwa ajili kuunganisha vinapatikana kwenye jukwaa la waendelezaji programu za kompyuta la Github.

Window 95, ambayo ilikuwa ni programu ya nne kutengenezwa tangu mwaka 1985 ilipotengenezwa Window 1, safari hii inakuja na programu mbalimbali ikiwemo Microsoft FrontPage, Netscape 2.0 na FrontPage Server, michezo ya kompyuta (gemu)  kama vile Doom, Wolfensterin 3D, A10 Tank Killer na Grand Prix Circuit.

Wakati Window 95 inaanza mwaka 1995 ilifanikiwa kutambulisha vitu vipya kwenye ulimwengu wa kompyuta kwa mara ya kwanza ambavyo vinatumika mpaka sasa ikiwemo Taskbar, Start Menu, na muonekano mzima wa programu endeshi ya Windows (GUI).

Huenda ikawa ni jambo jema kwa watumiaji wa kompyuta wenye umri mkubwa kidogo ambao walibahatika kutumia mfumo huo Tanzani mwishoni mwa miaka 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000.