Zijue App 42 zinazohatarisha betri la simu yako
Programu hizo zinasababisa betri ya simu kuisha kwa uharaka na zaidi, zinachochea matumizi makubwa ya intaneti huku zingine zikichukua taarifa binafsi za mtumiaji.
- App hizo ni pamoja na Du recorder na mini lite facebook
- Watumiaji washauriwa kuziondoa haraka iwezekanavyo
Dar es Salaam. Shirika la usalama wa kimtandao la ESET limeonya kuwepo kwa App 42 ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya betri ya simu pamoja na kuchochoea matumizi makubwa ya data (Internet) kwa mtu anayezitumia.
App hizo zinapatikana kwenye duka la mtandaoni la Google (Google playstore) na kwa mujibu wa ESET, programu hizo zinakuja na mfumo wa kimatangazo usio rasmi maarufu kama “adware”.
Programu hizo zinasababisa betri ya simu kuisha kwa uharaka na zaidi, zinachochea matumizi makubwa ya intaneti huku zingine zikichukua taarifa binafsi za mtumiaji.
ESET imtaja App hizo kuwa pamoja na Smart Gallery, Mini lite for Facebook, DU Recorder, Free Radio FM online na Water Drink Reminder.
Zingine ni App ambazo zinawezesha kupakua video kwenye mitandao ya kijamii isiyoruhusu kupakua kama Instagram. App hizo ni pamoja na SaveInsta na Free Video Downloader. Picha| Mtandao.
Zingine ni App ambazo zinawezesha mtu kupakua video kwenye mitandao ya kijamii isiyoruhusu kupakua kama Instagram na Twitter. App hizo ni pamoja na SaveInsta, Free Video Downloader, Free social video downloader, File Downloader, Video downloader,
Smart Notes for You, Tank classic, Heroes Jump, Solucionario, Ringtone Maker,MP4 video downloader na Free Top Video Downloader.
Zingine ni pamoja na zile za miito ya simu na michezo ya kwenye simu kama Ringtone Maker Pro, Basketball Perfect Shot, HikeTop+ na Flat Music Player.
zinazohusiana
Hata hivyo, baada ya Google kufikiwa na taarifa hizo imeziondoa baadhi ya App hizo kwenye duka lake la mtandaoni lakini bado inamhitaji mtumiaji pia kuziondoa kwenye simu yake kwani google haiwezi kufanya ivyo.
App ambazo bado zipo kwenye Playstore ni pamoja na hiketop+ nyinginezo huku baadhi kama Flat music player ikiwa ni kati ya zile zinazotengenezwa upya.
Hata hivyo, watumiaji wa mfumo endeshi wa IOS unaotumika kwenye simu za Apple pia wanakabiriwa na changamoto hizo kwani baadhi ya App hizo zipo kwenye duka la App store.
Wataalamu wa teknlolojia wanashauri kwa yeyote ambaye bado anatumia programu hizo kuziondoa kwenye simu yake haraka iwezekanavyo.