May 18, 2024

Wajasiriamali wafundwa njia za kupata mitaji

Washauriwa kuwa wakweli pindi wanapoomba mitaji kutoka katika wawekezaji mbalimbali ili waweze kufaniikiwa.

  • Washauriwa kuwa wakweli pindi wanapoomba mitaji kutoka kwa  wawekezaji mbalimbali ili waweze kufaniikiwa.
  • Wajasilimali wote hawana tofauti kwa kuwa wanahitaji kitu kimoja  tu manunuzi ya bidhaa zao au huduma zao
  • Waaswa kutumia mitandao ya kijamii kwa kutofautisha ukurasa binafsi na biashara.

Dar es Salaam.Ukosefu wa mbinu na mipango kabambe katika kutafuta mitaji  ni miongoni mwa matatizo mengi yanayo wakabili wajasilaimali wengi hapa nchini.

Kwa kuona changamoto hiyo Agapiti Manday mwanzilishi mwenza wa Tanzania Data lab (Dlab) amewapa elimu washiriki wa tamasha la wanawake kwenye teknolojia Tanzania  mwaka 2019 lililofanyika Buni ,Dar es Salaam,namna wanavyoweza kukabiliana na changamoto hizo ,ili waweze kuwavutia wawekezaji na kuwapa mitaji ya kuendeleza biashara zao.

“Ukiwa unaomba hela usiseme kuhusu matatizo kama hujaulizwa, kwa sababu watanzania tuna kasumba ya kuongelea matatizo kuliko mafanikio,” amesema Agapiti Manday.

Manday amewaambia washiriki hao kama wanataka kufanikiwa hasa katika kupata mitaji kutoka sehemu mbalimbali lazima waweze kujieleza vizuri kwa njia ya maandishi au kwa njia ya mdomo ili kuwashawishi mwekezaji  kuwapa mtaji au mkopo katika kuendeleza biashara.

Hata hivyo, amewatoa wasiwasi wajasiriamali hao kwa kutaka wajiamini na kujua kwamba katika ujasiriamali hakuna mjasiriamali mdogo au mkubwa kwasababu wote wanahitaji kitu kimoja manunuzi ya bidhaa zao au huduma.

Suala la ujasiriamali linahitaji mbinu mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzifanya uweze kufanikiwa na haina budi kila siku kujifunza.Picha| Zahara Tunda.

Manday amesema  lazima  mjasiriamali kuwa makini pale wanapoandika mawazo au  mipango kazi yake kwa ajili ya kuomba mtaji kwa mwekezaji kwa kusema ukweli mtupu kuhusu maisha yake bila kukwepesha chembe yoyote ya ukweli.

“Ukiwa unaomba mkopo kuwa mkweli sema unatimu ya watu wangapi sio mko sita unasema tupo wawili, unavunja uwaminifu mapema,” amesema Manday.

Pamoja na elimu hiyo ya kujipatia mtaji iliyotolewa kwa washiriki wa tamasha pia mdau wa masoko na ujasliamali amesema kuna haja ya wajasiliamali hao  kutumia mbinu mbalimbali za kujiongezea soko na kujitangaza zaidi.

Abdul Aziz mtaalam wa masoko kidigitali amewaambia wajasiriamali hao wanawake  kutumia mitandao ya kijamii katika kutangaza biashara zao, ila wanapaswa kuwa makini kutokuchanganya kurasa za biashara na za binafsi.

“Inabidi kuwa makini ukurasa wa biashara uwe wa biashara tu, ukianza kuchanganya na mambo yako binafsi wapo wateja wanaweza wasikupende wewe ila wakapenda bidhaa yako,” amesema Aziz.


Zinazohusiana: Wanawake msisubiri kubebwa fursa za teknolojia – Wadau

                           Facebook yaja na tovuti ya ‘usiri’ kuwasaidia wafanyabiashara kuelewa sera zake


Hata hivyo Aziz ameweka wazi biashara ya mtandaoni inahitaji umakini na uamnifu mkubwa  kwa  wajasiriamali  hasa katika kufikisha bidhaa ya mteja baada ya kununua  bila kuvunja makubaliano yao ya kibiashara, kwa sababu kupitia uwaminifu wateja wataongezeka na mtaji utakuwa.

“Hakikisha picha unayorusha mtandaoni kuhusu biashara yako inaendana na bidhaa halisi,” amesema Aziz.

Kwa upande wake mjasiriamali Brian Paul ame waasa kuwa sio kazi rahisi kama wanavyodhani kwa kuwa biashara inachangamoto nyingi.

”Kama wengine mnaona mnapenda kuajiriwa mfanye hivyo na kuhakikisha kuwa mnafanya kazi kwa bidii, huku akitoa rai kwa wajasilimali hao wanawake  kufanya vitu kwa kushirikisha.”, amesema Paul